AFARIKI BAADA YA KUCHAPWA NA WAZEE WA KIMILA - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, June 26, 2016

AFARIKI BAADA YA KUCHAPWA NA WAZEE WA KIMILA


Mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha Kandashi, wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro, Abedi Akyo (53), amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchapwa viboko na wazee wa kimila kwa tuhuma ya kujihusisha na wizi wa kuku.

Akielezea mazingira ya kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilfred Mutafungwa amedai kuwa Akyo alichapwa viboko 70 na wazee hao wa kimila wa Kimeru na Kimasai.

Mutafungwa amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mwezi uliopita wakazi wa Kata ya Karansi wilayani hapa walitoa uamuzi kuwa wanawake watakaovaa sketi fupi na vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno, wataadhibiwa kwa kuchapwa viboko 60 hadi 70.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here