Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria vikao kumi vya bunge kuanzia leo June 30 mwaka huu baada ya kubainika kunyosha kidole cha kati kwa wabunge baada ya kukiri mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka kwamba alifanya kitendo hicho. Hata baada ya kuhojiwa Mbunge Mbilinyi alishindwa kumtaja Mbunge wa CCM aliyedaiwa kumtukana ili nae achukuliwe hatua na kamati hiyo. Bunge limeridhia adhabu hiyo iliyotolewa na kamati.
Mbunge wa Ubungo Chadema Saed Kubenea amesimamishwa kuhudhuria vikao vitano vya bunge na Naibu Spika Dk Tulia Akson baada ya kubainika kusema uongo kwamba Waziri wa Ulinzi na JKT Dk Hussein Mwinyi ameingia Mkataba na kampuni ya China Henan International Cooperation Group Company wa ujenzi wa nyumba za JWTZ na nyumba ya Waziri huyo jambo ambalo sio kweli.
LAPF wakiwa tayari kabisa kuanza msimu wa maonesho ya biashara ya kimataifa Saba Saba 2016
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sababu za ushiriki wa Mfuko katika maonyesho ya biashara ya kimataifa (Saba Saba 2016).
Afisa Mifumo ya kompyuta kutoka Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Yohana Nyabili akitoa maelezo kwa mwanachama wa Mfuko pamoja na kumpatia taarifa ya michango yake mara baada ya mwanachama huyo kutembelea banda ya Mfuko kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa (Saba Saba 2016).
Timu ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF inayoshiriki maonyesho ya biashara ya kimataifa (Saba Saba) ikiwa ndani ya banda nadhifu ambapo huduma mbalimbali zinatolewa kwa wanachama na wadau mbalimbali wa Mfuko.
Banda la Mfuko wa Pensheni wa LAPF likionekana kwa nje likiwa na unadhifu wa hali ya juu, mbele ya banda ni timu ya maofisa wa LAPF wakiwa tayari kuhudumia wageni wote wanaofika katika banda la Mfuko kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa 2016.
Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya banda nadhifu la Mfuko huo katika maonyesho ya biashara ya kimataifa 2016.
No comments:
Post a Comment