China ndio taifa linalomiliki kompyuta bora zaidi duniani.
Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa ya hivi punde zaidi China inakompyuta bora na yenye nguvu zaidi duniani ya 93 petaflop Sunway TaihuLight.
TaihuLight imewekwa katika ofisi za National Supercomputing iliyoko Wuxi.
Katika kilele chake, kompyuta hii anaweza kufanya karibu mahesabu trilioni 93,000 kwa sekunde.
Kompyuta hiyo ina kasi mara mbili zaidi ya ile iliyokuwa ikiongoza ya Tianhe-2, pia kutoka China jarida la Top500 linasema.
Uweledi wake upo katika sekta ya uzalishaji, utabiri wa hali ya anga, utathmini wa data kubwa za mashirika kwa mujibu wa mtafiti Jack Dongarra.
Mashine hii inazaidi ya 'Nodes' 40,960 huku ikitumia mtambo wa programu maarufu ya Linux.
Kwa mara ya kwanza tangu orodha hii ianze, China imeipiku Marekani ikiwa na kompyuta 167 katika ya 500 bora, Marekani ina 165.
Marekani ina kompyuta nne kati ya 10 bora katika orodha hiyo ya Top500, wakati China ina mbili ambayo kwa sasa zinachukua nafasi ya kwanza na ya pili.
Nafasi zingine katika kumi bora zinachukuliwa na mashine kutoka Japan, Uswisi, Ujerumani na Saudi Arabia.
No comments:
Post a Comment