Diwani wa Kata ya Mtibwa (Chadema), Lucas Edwald Mwakambaya akiwa Kituo cha Redio cha Planet FM kukanusha tuhuma hizo.
Stori: Dustan Shekidele, Wikienda
MOROGORO: Yamemkuta! Diwani wa Kata ya Mtibwa, Jimbo la Mvomero mkoani hapa kwa ‘leseni’ ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Lucas Edwald Mwakambaya (38) ‘Rais wa Mtibwa’, amenaswa gesti akiwa na ‘kabinti’ kenye umri wa miaka 14 kisha kutiwa mbaroni.
Habari kutoka ndani ya jeshi la polisi mkoani hapa zilidai kwamba, diwani huyo alikamatwa juzikati ndani ya gesti iitwayo Baraka iliyopo Sultan Area.
Ilidaiwa kwamba, baada ya watu kumuona Lucas akiingia kwenye gesti hiyo na binti huyo waliwatonya polisi.
Wikienda lilipozungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Ulrich Matei kuhusu ishu hiyo alikiri kutokea.
“Polisi walipata taarifa kutoka kwa msiri mmoja kwamba katika nyumba hiyo ya kulala wageni, kuna mtu aliyeonekana na binti huyo ndipo walikwenda na kumkuta diwani huyo akiwa na binti huyo chumba namba 108 wakamkamata,” alisema Kamanda Matei.
Aliongeza kuwa, mtuhumiwa huyo alifikishwa Kituo cha Polisi cha Kati ambapo baada ya kutoa maelezo, aliachiwa kwa dhamana.
Hata hivyo, alipopata dhamana alikimbilia kwenye Kituo cha Redio cha Planet FM na kukanusha tuhuma hizo kupitia Kipindi cha Planet Morning akidai zina lengo la kumchafua kisiasa.
No comments:
Post a Comment