Imevuja! Kuyeyuka au kuharibika kwa ule ujauzito wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ‘Madam’ hivi karibuni kumetajwa na daktari kuwa ni matokeo ya tabia yake ya kukaidi ushauri wa kitaalam, Amani lina cha kuwapa wasomaji wake.
Hayo yalisemwa na mtu wa karibu we Wema (jina lipo) akizungumzia masharti ambayo daktari aliyepata kumtibu mrembo huyo aliyasema. Lakini pia, daktari mwingine wa jijini Dar, Dk. Fadhili Emily naye ameibuka na kuliambia Amani kuwa, Wema ana sababu 8 za mimba zake kuyeyuka akiwa anajua au hajui.
DAKTARI WA KWANZA
Mtu huyo wa karibu na Wema alisema mimba ambayo staa huyo aliifanyia shoo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kuyeyuka Februari, mwaka huu, ilitokana na sababu ya kugoma kutii masharti ya kitabibu.
SABABU YA KWANZA
“Vipimo vya kitabibu vilisema kuwa Wema alitakiwa kupumzika kwa muda mrefu ili kuilinda mimba hiyo kwani ilikuwa katika hatihati ya kutoka kama mhusika atakuwa ni mzururaji. Sasa Wema akiwa mjamzito alikuwa hakosi viwanja.”
USHAHIDI
Februari, mwaka huu, akiwa mjamzito, Wema alihudhuria tukio la uzinduzi wa Video ya Lupela iliyozinduliwa na Alikiba Salehe kwenye Hoteli ya Slipway, Oysterbay jijini Dar.
SABABU YA PILI
“Ilifika wakati, Wema alitakiwa kupewa bed rest (mapumziko ya kitandani) ili kulinda mimba yake. Hilo nalo likawa gumu kwake kukubaliana nalo. Ndiyo ikawa sababu ya mimba kutoka.”
SABABU YA TATU
“Sababu ya tatu, aliambiwa na daktari wake asifanye kazi ngumu, jambo ambalo lilikuwa likimshinda. Yeye si mtu wa kukubali kukaa tu muda wote. Hilo nalo lilichangia.”
Wema SepetuWema akiwa na mama yake mzazi
SABABU NYINGINE 5
Naye Dk. Fadhili, akizungumza na gazeti hili Jumatatu iliyopita, alisema sababu tatu ambazo zinadaiwa zilichangia mimba ya Wema kuyeyuka ni za kweli, lakini akasema Wema bila kujijua au akijua, mimba zake kadhaa zimeshatoka kwa vile wanawake wengi wenye matatizo ya kutoshika mimba, hushika na kutoka bila wenyewe kujijua na pia akaanika sababu za hali hiyo kumtokea mwanamke.
Lakini akasisitiza kuwa kuharibika kwa mimba ni tatizo ambalo linaweza kumkumba mwanamke yeyote, si Wema tu.
SABABU ZA KIMAUMBILE
“Sababu za mimba kutoka zenyewe zinatajwa kwamba ni tabia ya kurithi, yaani vinasaba ambavyo si vya kawaida. Kwa hiyo, kiumbe kinakuwa katika hali ambayo kwa asili mimba haiwezi kukua. Kama mtoto akizaliwa basi atakuwa na matatizo ya kimaumbile na kiakili.”
SABABU YA MUUNGANO
“Sababu nyingine ni kukosekana kwa yai lililorutubishwa. Katika kuumba, yai la mwanamke hukutana na mbegu ya mwanaume na zoezi la kiumbe kukua huanzia hapo kwa yai kujitenga mara mbili. Upande mmoja hutengeneza kondo la nyuma na kifuko cha kutunza maji na sehemu ya pili hutengeneza kiumbe au mtoto.
“Huwa inatokea sehemu ya kondo la nyuma inaendelea kukua wakati sehemu ya mtoto haikui. Katika hali kama hii, kama mama hajafanya vipimo kujua maendeleo ya mtoto, uwezekano wa mimba kutoka kabla ya kufikisha wiki 24 ni mkubwa.
“Lakini hili la muunganiko nasema pia kwamba, kwa mwanamke ambaye mimba yake inahofiwa kutoka, ni hatari kuendelea kukutana kimwili na mwanaume wake kwani uwezekano wa kutoka ni mkubwa.”
KUHUSU IDRIS
Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba walikuwa wakiendelea ‘kukutana’, lakini kipindi cha ujauzito wake, Wema na Mbig Brother, Idris Sultan uhusiano wao ulikuwa umekolea.
SABABU YA POMBE
“Sababu nyingine inayochangia kuharibika kwa mimba ni unywaji wa pombe kupita kiasi kwa mama mjamzito au kuvuta sana sigara,” alisema dokta huyo.
SABABU YA MAGONJWA
Sababu nyingine alizitaja kuwa ni magonjwa yanayoshambulia mwili wa mama na kiumbe wake tumboni kama vile malaria na kaswende.
SABABU YA KUTOA MIMBA
Daktari huyo alisema kuwa, mwanamke kutoa mimba mara kwa mara kunachangia kuharibika au kushindwa kunasa mimba baadaye.
“Lakini si lazima awe anatoa mimba mara kwa mara, mwanamke anaweza kutoa mimba mara moja tu ikiwa katika mazingira ya ukuaji salama. Hilo linaweza kuwa tatizo kubwa la mimba kutoka siku za usoni,” alisema.
USHAHIDI
Katika mahojiano na gazeti damu moja na hili, Risasi Jumatano mwaka jana, Wema alikiri kuwahi kutoa mimba moja tu ya aliyekuwa staa wa filamu za Bongo, marehemu Steven Kanumba.
WEMA ASAKWA
Mpaka juzi Jumanne, gazeti hili lilikuwa limetimiza siku saba za kumsaka Wema kwa ajili ya kupata vielelezo vyake kufuatia madai au maelekezo hayo ya daktari lakini bila mafanikio kwani hapokei simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, nao hakuujibu
Chanzo:GPL
No comments:
Post a Comment