ENGLAND IMESHINDWA KUONGOZA KUNDI B EURO 2016 - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, June 21, 2016

ENGLAND IMESHINDWA KUONGOZA KUNDI B EURO 2016


England imeshindwa kuongoza Kundi B la michuano ya Euro 2016 baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana na Slovakia katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo uliochezwa huko Saint-Etiene, Ufaransa.

Hodgson alifanya mabadiliko ya kuwapumzisha wachezaji wake sita wa kikosi cha kwanza, nahodha Wayne Rooney ambaye alikuwa chachu kwenye ushindi dhidi ya Wales pia alianzia benchi kwenye mchezo huo. Lakini kushindwa kupata ushindi dhidi ya Slovakia kunaifanya England kumaliza nafasi ya pili na huenda ikakutana na wakati mgumu kwenye mechi yake ya hatua ya 16 bora.

England walipata nafasi nzuri za kupachika mabao lakini golikipa wa Slovakia Matus Kozacik alikuwa makini kuokoa mchomo wa Jamie Vardy wa kipindi cha kwanza kabla ya kufanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa Nathaniel Clyne kipindi cha pili.

Rooney aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Jack Wilshere lakini haikusaidia kubali matokeo mbele ya Slovakia waliozuia kufungwa goli ili kupata pointi moja muhimu kwao.

Shuti la Dele Alli liliokolewa kwenye mstari na Martin Skrtel sekunde chache baada ya kuingia akitokea benchi.

England watasafiri hadi Nice ambako watacheza dhidi ya timu itakayomaliza nafasi ya pili kutoka Kundi F kati ya Hungary, Ureno, Iceland au Austria kwenye mchezo wa 16 bora Jumatatu ijayo.

Dondoo muhimu
  • England walipiga mashuti 29 (pamoja na yaliyokuwa-blocked) mashuti yao mengi zaidi kwenye fainali za michuano ya Ulaya tangu mwaka 1980.
  • Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa England kutoka 0-0 ndani ya mechi 15, mara ya mwisho kupata matokeo kama hayo ilikuwa dhidi ya Jamhuri ya Ireland June 2015.
  • Huu ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa Slovakia kupata clean sheet kwenye mechi zao saba za mashindano makubwa.
  • England wamefuzu hatua ya mtoano ya michuano ya Ulaya kwa mara ya nne baada ya kufanya hivyo miaka ya 1996, 2004 na 2012.
  • Nathaniel Clyne alitengeneza nafasi saba kwa England, akifikia rekodi yao ya kufanya hivyo kwenye mchezo mmoja ya mwaka 1980.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here