HAKI ZA BINADAMU WAONGEZEWA MAKALI NA NORWAY. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, June 23, 2016

HAKI ZA BINADAMU WAONGEZEWA MAKALI NA NORWAY.


Katika kuimarisha uhusiano mzuri baina ya Tanzania na Nchi ya Norway, balozi wa Norway nchini amekabidhi msaada wa shilingi bilioni 4.5 kwa Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ikiwa ni lengo la kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya kituo hicho.

Akizungumza na wanahabari balozi wa Norway nchini, Hanne Marie Kaarstad amesema kuwa msaada huo ni moja kati ya kutambua mchango wa kituo hicho katika utekelezaji wa majukumu yake ambapo kupitia ripoti zake imeonesha mchango wake mkubwa katika kuisaidia jamii dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini.

“ Tangu Norway ilipoanza kuisaidia LHRC mwaka 2004 hadi sasa wameonesha uwezo wao wa kuwa mstari wa mbele katika kuionesha jamii ni jinsi gani kituo hicho kilivyo na umuhimu kwa jamii na kimefanikiwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika Nyanja zote”. Alisema Balozi Hanne Marie

Kwa upande wake Mkurugenzi wa LHRC Dk. Hellen Kijo – Bisimba mara baadaya ya kupokea msaada huo amemshukuru Balozi huyo na kusema kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo utasaidia kituo hicho katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo kudai Katiba mpya ya Tanzania.

“Msaada huu ni kwaajili ya kuendeleza miradi iliyopo kwa ajili ya kazi za tume katika kupingana na ukatili wa aina yoyote ile pamoja na kudai mchakato wa Katiba Mpya ya Tanzania”. Alisema Bisimba

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here