HIVI NDIVYO WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WALIVYO ADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, June 22, 2016

HIVI NDIVYO WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WALIVYO ADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.  Doto James

Wizara ya Fedha na Mipango imeadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano na Watumishi wake, lengo likiwa ni kujadili mafanikio na changamoto wanazo kabiliana nazo mahali pa kazi.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James aliwataka Watumishi kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. John Magufuli katika kupambana na masuala ya rushwa, uzembe kazini na Watumishi hewa ambao wamekuwa wakiigharimu Serikali fedha nyingi katika kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Alisema Wizara inajipanga kuhakikisha inaboresha mazingira ya kazi kwa watumishi hasa kwa wale wenye ulemavu kwa kuwajengea miundombinu rafiki sehemu za kazi ili kuongeza ufanisi kazini.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo katika maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma kwenye ukumbi wa mikutano hazina.Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Gideon Manambo.

“Wizara pia inafanya vizuri katika masuala ya usawa wa kijinsia kwa kuwa na idadi inayoridhisha ya wanawake hasa katika ngazi za maamuzi, ikiwa ni pamoja na kuwa na Manaibu Katibu Wakuu wawili wanawake” . Alisisitiza James

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Gideon Manambo alisema kuwa, watumishi wanatakiwa kufanya kazi kwa ufanisi na kwa bidii ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya maendeleo ambayo yanahitaji watendaji wenye weledi wa kutosha ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.

Kwa upande wa watumishi wa Wizara, wameuomba uongozi kuhakikisha kunakuwepo na vitendea kazi vya kutosha ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa na matokeo chanya ambayo yatasaidia kutatua matatizo yanayowakabili wananchi.

Maadhimisho hayo yamefanyika kufuatia utaratibu mpya uliowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano ambapo uliagiza Wizara pamoja na Taasisi kuadhimisha Wiki hiyo kwa kutatua matatizo ya watumishi wa Umma pamoja na wananchi kwa ujumla katika maeneo yao ya kazi.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here