Simba ipo katika harakati za kuimarisha kikosi chao kwa kuhakikisha hawafanyi makosa katika usajili kipindi hiki ambacho dirisha la usajili limefunguliwa.
Uongozi wa Simba umesema kipaumbele chao cha kwanza katika kipindi hiki cha usajili ni kocha, wanataka wampate kocha mwenye rekodi nzuri ambaye pia atawasaidia katika kuwasajili wachezaji wazuri, Mwenyekiti wa klabu hiyo Evans Aveva amebainisha hilo kwa kusema lengo ni kushirikiana na kocha huyo katika kufanya usajili ambao utakuwa ni wa uhakika.
"tunaona suala la kocha liwe namba moja, wachezaji tayari tumeanza kusajili vizuri lakini itapendeza kama tutakuwa na ushirikiano wa karibu na mkuu wa benchi la ufundi maana wao ndiyo wataalamu zaidi yetu." alisema Aveva.
Bosi wa kamati ya usajili Zacharia Hans Poppe alisafiri kwenda nchini Zimbabwe kujaribu kuzungumza na kocha anayeifundisha timu ya taifa ya Zimbabwe, Kalisto Pasuwa lakini juhudi hizo ziligonga mwamba na kumkosa kocha na kuamaua kuongeza kasi za kusaka kocha mwingine.
No comments:
Post a Comment