Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula (katikati) akizindua kitabu hicho cha ‘Majipu ya Nchi Yetu’ cha Amos Siyantemi.
…Akiwa na kitabu hicho.
Mwandishi wa kitabu hicho, Amos Siyantemi, akisoma taarifa kwa wanahabari (hawapo pichani).
Wanahabari wakichukua tukio hilo.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Philip Mangula, leo amezindua kitabu cha Mwenyekiti wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo, Amos Siyantemi, kijulikanacho ‘Majipu ya Nchi Yetu: Tushirikiane Kuyatumbua’.
Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanahabari kutoka vyombo vya habari mbalimbali.
Akizungumza na wanahabari katika hafla hiyo, Siyantemi alisema maudhui ya kitabu hicho yanachochea moyo wa uzalendo na uwajibikaji kwa watendaji, viongozi na wananchi kwa ujumla.
Alisema kitabu hicho amekiandika kulenga juhudi mbalimbali za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika utendaji kazi wake huku akitoa wito kwa Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya sasa ya awamu ya tano inavyotumbua majipu na kuitekeleza kwa vitendo falsafa yake ya HAPA KAZI TU.
Siyantemi aliwaomba Watanzania wote kwa pamoja kuwa na dhamira ya kweli na utashi wa kisiasa katika kumuunga mkono na kumpa ushirikiano rais kwenye juhudi zake za kuijenga Tanzania na Afrika mpya kwa ujumla.
Naye Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula, alimpongeza mwandishi huyo kwa kuweka dhamira yake juu ya mambo mbalimbali yanayofanywa na Rais Magufuli, hususani ufuatiliaji wa watumishi hewa, rushwa na dhuluma kwa kuweka kumbukumbu ya maandishi ndani ya kitabu hicho kuhusu mambo hayo.
No comments:
Post a Comment