Refa mmoja raia wa Sweden, alimpa kwa mpigo kadi mbili za njano mwanasoka Adam Lindin Ljung-kvist, akiwa uwanjani, kwa kosa la kutoa hewa mbaya.
Mchezaji huyo alipokuwa katika harakati za kushangaa kuhusiana na hatua ya refa huyo, alipigwa kadi nyekundu na kuondolewa uwanjani.
Refa huyo ametaja kitendo cha Adam cha kutoa ushuzi , kama tabia isiyo ya mchezaji. Lakini kulingana na Adam, alidhani alikuwa akifanya hivyo kimaumbile tu na wala hakuwa na nia ya kumchafulia refa hewa.
Taarifa hiyo imeibua malumbano makubwa kote duniani katika mtandao wa kijamii, huku wengine wakisema kuwa hiyo ni mara ya kwanza kwa mchezaji soka kupigwa kadi nyekundu kwa sababu ya kuchafua hewa.
Amesema kuwa ameshangazwa sana na refa kumtimua, huku akiongeza kuwa, kocha na wachezaji wenzake hawakuamini walipomuona akirejea katika eneo la wachezaji wa ziada na kuwaambia kuwa amepigwa kadi nyekundi kwa “kushuta.”
Adam, mwenye umri wa miaka 25 anaichezea timu ya Pershagen SK, inayo burura mkia katika ligi kuu nchini Sweden.
No comments:
Post a Comment