MCHEZAJI MZEE ZAIDI DUNIANI AWEKA REKODI MPYA YA UFUNGAJI - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, June 21, 2016

MCHEZAJI MZEE ZAIDI DUNIANI AWEKA REKODI MPYA YA UFUNGAJI


Nywele zake zimebadilika rangj na miaka imechukua miguu yake lakini akiwa na miaka 49 Kazoyushi Miura, Jumapili alionesha kwamba bado hayukotayari kustaafu baada ya kuweza kuvunja rekodi yake mwenyewe ya kuwa mchezaji mzee zaidi kufunga goli kwenye Ligi ya Japan.

‘Kazu’ kama anavyojulikana akicheza msimu wake wa 31 kama mchezaji alifunga goli la kichwa lililoitanguliza timu yake Yokohama FC katika dakika ya 22 ya mchezo dhidi ya FC Gifu kwenye daraja la Pili la Ligi ya Japan, japo timu yake ilifungwa 2-1 katika mechi hiyo.

Kazu aliweza kufunga goli hilo akiwa na miaka 49, miezi mitatu na siku 24. Mchezaji huyu mzee zaidi duniani aliwaambia waandishi wa habari baada ya mechi kuwa bado ana njaa ya magoli ingawa majeraha yanamsumbua sana siku za hivi karibuni.

“Nina furaha sana,” alisema Kazu, “Nilikuwa najisikia vizuri sana mazoezini na nilihisi kuwa nitapata goli moja. Kipigo hiki kinanihuzunisha na nahitaji kufunga magoli mengi zaidi kiukweli.”

Mchezaji huyu wa zamani wa timu ya taifa ya Japan hakufanikiwa kucheza kombe la Dunia licha ya kucheza mpira muda mrefu sana, japo ana rekodi nzuri kwenye timu ya taifa ya Japan ambapo amefanikiwa kufunga magoli 55 katika mechi 89.

Miura alikuwepo katika uzinduzi wa msimu wa kwanza wa Ligi hiyo ya Japana iitwayo J-league mwaka 1993 na alikuwa mchezaji kwenye timu ya Verdy Kawasaki ambayo ilitwaa ubingwa wa kwanza wa ligi hiyo.

Akiwa na miaka 15, Miura alisafiri peke yake kuelekea nchini Brazil ambapo alichezea klabu mbalimbali na hata akafanikiwa kuchezea klabu ya Neymar ya zamani Santos.

Miuri alirudi Japan miaka minne baadaye ambapo alichezea Yomiuri FC na baadae akachezea klabu za Genoa na Dinamo Zagreb barani Ulaya.

Miuri aliisaidia Japan kufuzu kombe la Dunia la mwaka 1998 ila kocha wake kwa wakati huo Takeshi Okada alimkata kwenye timu dakika za mwisho kitendo ambacho mashabiki wa mpira wa Japan hawajakisamehe hadi leo hii.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here