MMILIKI WA TIMU YA TP MAZEMBE AHUKUMIWA KIFUNGO JELA. MIAKA.. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, June 22, 2016

MMILIKI WA TIMU YA TP MAZEMBE AHUKUMIWA KIFUNGO JELA. MIAKA..


Mgombea urais wa upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi, amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela kwa kununua nyumba kinyume cha sheria kwenye mji ulio mashariki mwa nchi wa Lubumbashi. 

Pia alipigwa faini ya dola milioni 6. 

Katumbi hakuwa mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo, baada ya kusafiri kwenda afrika kusini kupata matibabu siku moja baada ya serikali kutangaza waranti ya kukamatwa kwake kwa mashtaka tofauti. 

Analaumiwa kwa kuwaajiri mamluki wa kigeni ili kupanga njama dhidi ya serikali.

Katumbi amekosoa hukumu hiyo, akisema kuwa ni jaribio la kutaka kuchelewesha kampeni yake ya kutaka kumrithi Rais Joseph Kabila mwezi Novemba.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here