WANANCHI katika kijiji Kaseke kata ya Kasami wilayani na Mkoani Geita wamekubwa na taharuki na wasiwasi mkubwa mara baada ya Grace Saidi( 20) Kujifungua mtoto wa kiume mwenye vichwa viwili vinavyofanana sura.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jumapili majira ya saa sita usiku katika katika kituo cha afya katoro alikwenda kujifungua muda mfupi baada ya kupata uchungu.
Channel Ten ilifika kijijini hapo na kushudia viumbe hao huku mamia ya wananchi kutoka kila kona wakifika na kushudia tukio hilo na hapa mashuhuda wakaeleza ilivyokuwa.
Baba mzazi wa mtoto huo Stefano Lugisha amesema pamoja na mke wake kujifungua mtoto huyo lakini ana imani kama ni mipango ya mungu kama amavyoeleza.
Diwani wa kata hiyo Andrea Karamura pamoja na mwenyekiti wa kijiji Zakaria Lukas wamewataka wananchi wao kutoliusisha tukio hilo na imani za kishirikina.
Akiongea kwa njia ya simu mganga wa kituo hicho aliyempokea mama huyo na kumzalisha Peter Janga amedhibitisha kutokea kwa hilo na kwamba uchunguzi wa kina unafanyika ili kubaini nini tatizo kwa mama huyo ambaye huo ulikuwa ni uzao wake wa kwanza na kuongeza kuwa kiumbe hicho kilipoteza maisha baada ya muda mfupi.
No comments:
Post a Comment