NAIBU SPIKA AKABIDHIWA RIPOTI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015 BUNGENI MJINI DODOMA - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, June 30, 2016

NAIBU SPIKA AKABIDHIWA RIPOTI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015 BUNGENI MJINI DODOMA

Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekabidhiwa ripoti ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 Bungeni mjini Dodoma leo.

Akizungumza wakati akipokea Ripoti hiyo Naibu Spika amesema kuwa ripoti hiyo ni muhimu kwa Bunge na ni kiashiria cha ushirikiano mzuri kati ya Bunge na Tume hiyo.

“Ushirikiano uliopo kati ya Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni mzuri na kwa upande wangu natumaini tutaendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali,” alisisitiza Mhe. Dkt.Tulia.

Akizungumzia majukumu ya Bunge naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia amesema kuwa Bunge la kumi na moja limetimiza majukumu yake vyema hali itakayochochea maendeleo hapa nchini katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amepongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tume hiyo na Bunge kama mdau muhimu na kuahidi kuuendeleza kwa maslahi ya pande zote.

Ziara ya Tume hiyo pamoja na kukabidhi ripoti hiyo kwa Naibu Spika ililenga kuwajengea uwezo wajumbe wa Tume hiyo kuhusu majukumu ya Bunge ambapo wajumbe hao walitembelea maeneo mbalimbali ya Bunge.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekabidhi ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson ikiwa ni ishara ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akikabidhi ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson Bungeni Mjini Dodoma mara baada ya Kuirishwa kwa Bunge jana.


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva na ujumbe wake wakiangalia moja ya vitabu vilivyopo kwenye maktaba ya Bunge wakati wa Ziara yao Bungeni mjini Dodoma.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa kwenye picha ya Pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Ujumbe wake mara baada ya ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma leo.kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva na kulia Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahamud Hamid.


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akiongoza ujumbe wa tume hiyo kwenye viwanja vya Bunge leo wakati wa Ziara ya kutembelea Bunge na kuwasilisha ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here