NAIBU SPIKA WA BUNGE DK TULIA ASHIRIKI KAMPENI YA MEDIA CAR WASH DODOMA LEO - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, June 25, 2016

NAIBU SPIKA WA BUNGE DK TULIA ASHIRIKI KAMPENI YA MEDIA CAR WASH DODOMA LEO


Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ashiriki kampeni ya Media Car Wash mjini Dodoma leo.


 Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akiosha gari la Mbunge wa Nanyamba, Abdallah Chikota wakati wa kampeni ya Media Car Wash ya kuchangisha fedha za kusaidia wanahabari kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

.

Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja akisalimiana na Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani wakati wa harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini.
 
 

Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin Thompson akizungumza na baadhi ya wabunge na wageni mbalim bali kuelezea lengo la kampeni hizo asubuhi njini Dodoma. 

 

Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza kuwapongeza waandaaji wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani.

 

Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto (kushoto) na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kulia) wakishiriki zoezi la kuosha magari kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ Dodoma leo.


Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel na Mkongwe wa Bongo Fleva Inspector Haroun wakiosha moja ya magari yaliofika kuoshwa kwa ajili ya harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here