NGASSA AUKUBALI MZIKI WA YANGA. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, June 23, 2016

NGASSA AUKUBALI MZIKI WA YANGA.


Mrisho Ngassa Mtanzania anayechezea klabu ya Free State ya nchini Afrika Kusini amepongeza uwezo mkubwa waliouonyesha Yanga kwenye mechi yao dhidi ya MO Bejaia.

Ngassa ambaye yupo likizo kwa sasa amesema Yanga walicheza vizuri sana katika mchezo huo huku akisema kilichowaangusha ni kushindwa kuzitumia nafasi nyingi za magoli walizozitengeneza kwenye mchezo huo.

"Walicheza vizuri sana na walitengeneza nafasi nyingi lakini kwa bahati mbaya tu walishindwa kuzitumia nafasi hizo kufunga magoli. Walipambana hadi dakika za mwisho wakitaka kusawazisha goli hilo, kilikuwa ni kiwango kizuri sana." alisema Ngassa mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga.

Yanga sasa ina kibarua kizito dhidi ya TP Mazembe mchezo utakaopigwa Jijini Daresalaam Juni 28, 2016.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here