NIONAVYO MIMI: TP MAZEMBE WALISTAHILI USHINDI MBELE YA YANGA - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, June 28, 2016

NIONAVYO MIMI: TP MAZEMBE WALISTAHILI USHINDI MBELE YA YANGA


Mechi ya Kundi A kati ya wenyeji Yanga dhidi ya TP Mazembe ilikuwa ni moja kati ya mechi inayopendeza kutazama, wachezaji wa timu zote walionesha viwango vizuri licha ya Mazembe kwazidi Yanga kwa baadhi ya vitu na kupata ushi wao wa pili katika kundi hilo la michuano ya kombe la shirikisho Afrika ikiwa ni hatua ya makundi.

Kama uliungalia mchezo kwa jicho zuri utakubaliana na mi kwamba uzoefu mkubwa wa wachezaji wa Mazembe kwenye michuano ya kimataifa ulikuwa ni faida kubwa kwao kupata ushindi mbele ya Yanga ambayo Juma Mahadhi, Geofrey Mwashiuya, Anthony Maheo na wengine ndiyo wanacheza kwa mara ya kwanza.

Mazembe ni timu iliyojengwa kwa muda ikiwa na wachezaji walioshibana kwa muda sasa na wenye uzoefu na mashindano ya Afrika, lakini wakati huo kumbuka kwamba Yanga ilikuwa inacheza na bingwa wa ligi ya vilabu bingwa Afrika mwaka 2015.

Kuna mengi ya kuzungumza hapa lakini acha niende moja kwa moja kwenye baadhi ya mambo ambayo yamechangia Mazembe kupata matokeo kwenye mchezo wao wa ugenini dhidi ya Yanga.

Wachezaji wenye ubora

Golikipa wao Sylvain Gbohoud Guelassiognon ni golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Ivory Coast, alikuwepo golini kwenye kikosi kilichotwaa ubingwa mataifa ya Afrika. Hapa unatakiwa kujiuza tayari amekutana na mikikimikiki ya ma-striker wanagapi? Bila shaka majibu utakuwanayo mwenyewe.

Anamkalisha benchi Kidiaba ambaye miezi michache iliyopita ametoka kwenye fainali ya kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa Afrika anayecheza ligi za ndani, tuzo ambayo ilitwaliwa na mtanzania Mbwana Samatta wakati huo akiwa anaitumikia TP Mazembe.

Mlinzi wa kushoto na nahodha wa Mazembe Jean Kasusula, ameicheza mechi ngapi ngapi kubwa na zenye presha ya hali ya juu na tayari amekutana na wachezaji wa kila aina wenye uwezo mkubwa ndani na hata nje ya mipaka ya Afrika.

Licha ya kutofunga bao, Thomas Ulimwengu alikuwa kwenye kiwango cha juu kwenye idara ya ushambuliaji ya Mazembe na ameonesha kitu cha ziada alichonachi na kwa jinsi gani Mazembe wananufaika kwa uwepo wake katika klabu yao. Unamfahamu Ulimwengu ni mzuri kwa kutumia nguvu na kasi yake na mara kadhaa alimsumbua Kelvin Yondani.

Eneo la kiungo

Haruna Niyonzima na Thaban Kamusoko walitulia na walijitahidi kwa kiasi kikubwa kupiga pasi lakini pasi zao nyingi zilikuwa haziendi mbele na kuleta hatari kwenye goli la Mazembe. Ikumbukwe Mazembe wao walikuwa wanacheza ugenini na walikuwa wakihitaji matokeo, hivyo walikuwa wanacheza kwa mipango ili kupata pointi tatu kitu ambacho kilikuwa muhimu kwao na siyo kuifunga Yanga idadi kubwa ya magoli kama baadhi ya watu walivyotarajia.

Uzoefu unawapa faida TP Mazembe

Wao wanachotambua ni umuhimu wa kumaliza katika nafasi mbili za juu ili kufuzu hatua ya nusu fainali, kwahiyo ni lazima utengeneze mipango mapema kwamba nyumbani tunapata pointi tatu, tunazipataje hizo pointi tatu? Tunakwenda kucheza ugenini, tunavyocheza nymbani na ugenini ni michezo miwili tofauti ambayo inahitaji mbinu tofauti.

Unapocheza ugenini unahitaji kuwa mwepesi sana katika kumsoma mpinzani wako anachezaje na unamdhibiti vipi, kumuharibia mipango yake na kumchanganya ili wasiweze kutekeleza mipango yao waliyokuwa wamejiwekea. Mwisho wa siku kwa uzoefu waliokuwa nao Mazembe na plani waliyokuja nayo Mazembe, haikuwa ni ya kushambulia sana kwa walioutazama mchezo huu watakuwa ni mashahidi katika hili.

Lakini unaweza ukajua kuwa, walipanga endapo watapata nafasi ya kushambulia lazima watasababisha Yanga wafanye makosa na wao waitumie fusra hiyo kuweza kufunga. Na ndicho kilichotokea, mashambulizi ya hatari yaliyofanywa na Mazembe golini kwa Yanga ni machache na Yanga wakafanya kosa hilo na kilichotokea ni Bope kuwaadhibu.

Baada ya kufunga bao hilo, TP Mazembe wakarudi nyuma na kumwacha Ulimwengu mbele na kuanza kuwagongagonga wachezaji wa Yanga na hapo utasema jamaa walikuwa wanacheza rafu lakini si hivyo, walikuwa wanatumia nguvu nyingi kitu ambacho wachezaji wa Yaga walishindwa kupambana hasa pale ilipotokea vita ya mtu mmoja kwa mmoja.

Kwahiyo lazima tukumbuke Mazembe ni watu wanaojua namna ya kucheza mechi na siyo kuchezea mpira, lazima ujue kuna kuchezea mpira na kucheza mechi kwa ajili ya timu kupata matokeo.

Yanga wamekuwa wanatumia krosi kutengeneza nafasi ya kufunga magoli, lakini kwenye mchezo dhidi ya Mazembe kama uliufatilia vizuri, hakuna krosi ya juu hata moja ambayo iliwapita wachezaji wa Mazembe na kuchezwa na mchezaji wa Yanga. Mipira yote ya juu ilikuwa inaishia kwa wachezaji wa Mazembe kutokana na vimo vyao ukilinganisha na wale wa Yanga, hiyo iliwafanya wawe salama katika kulinda goli lao.

Pongezi kwa waamuzi

Nimsifu mwamuzi wa mchezo huu kwasababu alikuwa vizuri kwa mfano, kuna tukio la Kelvin Yondani kumwangusha Ulimwengu kama mwamuzi asingekuwa makini angewapa penati Mazembe lakini alikuwa makini na alikuwa na uhakika kwa kila uamuzi alioufanya. Tukio jingine lilimhusisha Kamusoko kumfanyia tackling Ulimwengu, Kamusoko alifanikiwa kuuchukua mpira miguuni kwa Ulimwengu lakini benchi zima la TP Mazembe lilisimama likilalamika kwanini mwamuzi hakutoa penati.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here