Mkazi wa Belarusia akiwa ofisini.
BAADHI ya wananchi wa Belarusia wamekuwa wakienda makazini wakiwa uchi, na baadhi yao wakitupia picha mtandaoni zikiwaonyesha wakiwa uchi kutimiza kauli ya rais wao aliyoitoa siku za hivi karibuni.
Alexander Lukashenko (61).
Kiongozi wa taifa hilo, Alexander Lukashenko (61), anatajwa kama dikteta pekee barani Ulaya ambapo amekuwa rais wa Belarusia toka mwaka 1994 hadi sasa. Lukashenko analaumiwa na watetezi wengi wa haki za binadamu kwa kuminya uhuru wa wananchi wake. Anahesabika kama mtawala dikteta aliyebakia barani Ulaya. Nchi ya belarusia inapakana na Russia, Ukraine, Poland, Lithuania and Latvia.
Lukashenko aliteleza wakati akifungua mkutano wa uwekezaji ambapo alitamka: “Kuwekeza katika tenknolojia ya kisasa, kuruhusu ubinafshaji na kukaribisha wawekezaji, vyote vitatusaidia kama taifa tusonge mbele. Na tayari teknolojia imetupa urahisi wa kutekeleza mahitaji yetu kiufasaha na sasa mtu anaweza kufanya kazi akiwa ‘undressed’ huru”.
Matumizi ya neno ‘undressed’ ndilo lililowababaisha baadhi ya waliolisikia ambapo kwa maana ya kinahau linamaanisha ‘kutovaa nguo au kuwa uchi’, wakati kwa maana halisi linamaanisha ‘kuwa huru’.
Akihojiwa na kituo cha gazeti la Observer, Doroshenko Kostyantyn alisema: “Hatuwezi kupingana na kauli ya rais, lazima twende kazini tukiwa uchi, kutimiza matakwa ya mkuu wetu wa nchi”.
Wananchi wa Belarusia wakiwa utupu.
Wananchi wengi wa Belarusia wamechoshwa na vitendo vya matumizi ya mabavu katika utawala vya Lukashenko. Kwa kauli yake hiyo wananchi walio wengi wanatumia mitandao ya kijamii kujipiga picha wakiwa uchi huku wakitamka bayana wanafanya hivyo kutimiza matakwa ya rais wao.
Wananchi wengi wanamwona rais wao kama kituko akiwa kama kiongozi mkuu wa taifa, huku akiteleza mara kwa mara kutamka maneno mazito. Lukashenko aliwahi kutamka ‘ni bora kuwa dikteta kuliko kuwa shoga au kusapoti ushoga’. Kwa Wabelarusia hakuna atakayeisahau kauli hiyo na tayari wameanza kuitekeleza kwa kasi.
Wachambuzi mbalimbali wa kimataifa wanamwona kiongozi huyo kama mtu aliyeanza kupoteza umakini wa kuzungumza mbele ya raia wake, hali inayosababisha kukosea mara kwa mara au kutamka vitu visivyo na mantiki katika jamii.
Wananchi wengi wanatekeleza suala hili ambapo lengo lao kuu ni kumfikishia ujumbe rais wao kwamba amechoka na anahitaji kuachia nafasi kwa wengine waongoze.
No comments:
Post a Comment