SERIKALI YAPOKEA MSAADA WA MADAWATI 300 TOKA UBALOZI WA KUWAIT NCHINI TANZANIA. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, June 22, 2016

SERIKALI YAPOKEA MSAADA WA MADAWATI 300 TOKA UBALOZI WA KUWAIT NCHINI TANZANIA.

Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa madawati 300 toka Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya kutatua tatizo la uhaba wa madawati katika shule za msingi hapa nchini.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga kwa niaba ya serikali alisema kuwa amesema kuwa kupokea madawati hayo ni sehemu ya kutekeleza wito wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
“Waziri Mkuu alitutaka sisi katika nafasi zetu tuwashirikishe wadau mbalimbali ili kuweza kutekeleza adhma ya serikali ya kutatua tatizo la wanafunzi kukaa chini ili waweze kupata mazingira bora ya kupata elimu, alisema Balozi Maige.
Balozi Maiga aliongeza kuwa Kuwait iko tayari kuisaidia nchi ya Tanzania kwa kuwajengea uwezo wataalam toka Tanzania kwa kuwapa elimu ya mafuta na gesi kwani Kuwait ina uzoefu mkubwa katika sekta ya mafuta na gesi. 
Naye Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem alisema kuwa Serikali ya Kuwait itaendelea kutoa misaada kwa serikali ya Tanzania kadri itakavyowezekana pindi pale itakapohitajika.


Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akikabdhi msaada wa madawati kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Maiga akitoa neno la shukrani kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem wakati akipokea msaada wa madawati toka kwa balozi huyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem (katikati) akikabdhi msaada wa madawati kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima mapema hii leo jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem (katikati) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (kulia) wakiwa wamekalia madawati ambayo yametolewa msaada kwa serikali ya Tanzania, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima mapema hii leo jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (Katikati aliyekaa) kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem na kulia ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi na Wakurugenzi toka wizara hiyo mara baada ya kupokea msaada wa madawati toka ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here