Asalamu aleikhum,
Ijumaa ya juzi Kuna Kundi la Jeshi na Polisi walikwenda katika Kijiji cha Kiungoni Pemba na kufyatua Risasi nyingi juu. Wananchi waliokuwa katika maduka yao waliingiwa na khofu nakukimbia huku Wakiacha Maduka yao wazi- Vikosi hivyo vya Ulinzi Ndipo walipopata nafasi yakuingia Ndani ya Maduka ya Wananchi na Kuiba Vyakula, Nguo, na bidhaa Nyengine.
katika kipindi cha October hadi sasa kumekuwa na Vijana wengi wa Kibara na Kutoka Unguja Wamekuwa Wakiva,mia Vijiji vya Pemba na kufanya Uharibifu. Vijana hao wanatumia Nguo za Kijeshi na Hujiita kwamba Wako katika Kazi maalumu huko Pemba.
Kuna Vijana 4 Walikutwa katika Nyumba Moja ambayo iko Pondeani na wanaishi humo kama Wanyama. Nyumbo hiyo Inamilikiwa na Mzee mmoja kutoka KIlwa Tanganyika ambae alihamia Pemba miaka ya 80 kwa ajili ya Uhunzi. Na hivi sasa anakodisha nyumba yake kwa Wanachama wa Maskani za CCm ambao huletwa Pemba kwa ajili yakuharibu Mashamba ya Mikarafuu na kuchoma choma vitu, kuuwa, kuiba na kupiga watu mikwaju.
WITO:
Tunawaomba Wananchi wa Pemba hasa majimbo kama ya Mkoroshoni Wafanye Doria za Usiku usiku kwani baadhi ya Vijana hao hivi sasa Wamehamia Nyuma ya Mji wa Mkoroshoni , kuelekea Pondeani.
No comments:
Post a Comment