SIKU KOCHA WA WEST HAM UNITED HARRY REDKNAPP ALIMPOCHEZESHA SHABIKI KWENYE MECHI - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, June 21, 2016

SIKU KOCHA WA WEST HAM UNITED HARRY REDKNAPP ALIMPOCHEZESHA SHABIKI KWENYE MECHI


Soma stori hii ikihadithiwa na kocha wa zamani wa Tottenham na West Ham Harry Redknapp kuhusu siku aliyomchezesha shabiki kwenye mechi.

Mwaka 1994 katika klabu ya West ham tulikuwa na mechi mbili za kirafiki katika usiku mmoja. Timu moja ilienda kucheza Billirecay na mimi nilichukua timu moja kwenda kucheza na timu yangu ya zamani Oxford.

Mechi ilipoanza tu jamaa mmoja aliyekuwa amekaa kwenye viti vya mashabiki karibia na benchi langu la ufundi alianza kupiga kelele kwenye sikio langu. Hakuwa mbaya na wala hakusema maneno mabaya. Alikuwa ameveaa t shirt na bukta na kila sehemu ya mwili wake ilikuwa imepigwa tattoo za klabu ya West Ham. Huyu jamaa alikuwa hamkubali hata kidogo mshambuliaji wangu kwa wakati huo Lee Chapman.

“Harry umempanga tena mbele Chapman!, nakuomba usimchague punda tu huyo hana mchango wowote,” alisema huyo shabiki.

Basi ikaendelea hivyo, jamaa aliendelea kunisumbua. Nilifanya mabadiliko mawili half-time na nikafanya mabadiliko mengine tena, kipindi cha pili kilipoanza na sasa nilibakiwa na wachezaji wangu kumi na moja tu waliokuwa wanacheza uwanjani na kama ilipangwa vile mchezaji wangu mmoja akapata majeraha. Sikuwa na kingine cha kufanya nikamgeukia yule shabiki.

“ Wewe si unaongea sana, unaweza kucheza vizuri kama unavyoongea?,” nilimuuliza

“Aaah nachojua mimi nikwamba nimemzidi Chapman,” alijibu huyo shabiki.

“Haya basi vaa jezi yako”, nilimwambia

“ Unamaanisha nini?,” aliuliza,

“Leo unaichezea West ham,” nikamjibu.

Alirudi kapiga uzi na akasimama karibia na uwanja, “Unacheza wapi?” nilimuuliza .

“Kule mbele,” akajibu.

“Haya basi tutaona kama kweli umemzidi Chapman,” nilimwambia.

Basi jamaa akaingia uwanjani. Mtangazaji wa Oxford alinifuata na akataka kujua ni nani yule aliyeingia sasa hivi “Hivi wewe hukuangalia kombe la Dunia enh, yule ni Tittishev wa Bulgaria. Alifunga magoli matatu kule.” Nilimjibu.

“Aaah kumbe Tittishev, alafu nilihisi ni yeye tu,” alijibu yule mtangazaji.

Yule Shabiki alifunga goli kwenye ile mechi. Hatukuamini. Alikimbia uwanja mzima utafikiri alitoka kushinda hilo kombe la Dunia kweli tulikuwa tunacheka sana kwenye benchi la ufundi.

Mwisho wa mechi wachezaji wangu wote wali-sign jezi yake na aliandikwa kwenye gazeti siku inayofuata akionesha kicheko hicho ambacho hujawahi kupata kuona kwenye maisha yako na jamaa alikuwa sahihi kweli siku ile alimzidi kiwango Lee Chapman.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here