UEFA EURO 2016: URENO WAZIMA NDOTO ZA CROATIA , WASHINDA 1_0 - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, June 25, 2016

UEFA EURO 2016: URENO WAZIMA NDOTO ZA CROATIA , WASHINDA 1_0

Mchezo baina ya timu ya Taifa ya Croatia dhidi ya timu ya Taifa ya Ureno katika michuano ya Uefa Euro 2016, umemalizika kwa timu ya Ureno kusonga mbele kwa ushindi wa bao 1-0.

Awali mchezo huo ulimalizika kwa dakika 90 za mchezo kwa kutoka 0-0 na kuingia hatua ya pili ya lala salama ambazo ziliongezwa dakika 30. Mchezo huo uliokuwa mkali kwa pande zote mbili, Croatia watajijutia wenyewe kwa kukosa nafasi nyingi lakini Ureno walitumia nafasi hiyo ya kipekee na kuweza kupachika bao hilo ambalo lilitafutwa kwa taabu na mchezaji nyota wa timu hiyo. 

Cristian Ronaldo ambaye pia alipiga shuti lake na kuokolewa na kipa wa Croatia na mpira huo kuja kumpata mchezaji huyo wa Ureno aliyetokea benchi, Quaresma na kupachika bao hilo kwa kichwa na kufanya mchezo huo kuwa Croatia 0-1 Ureno.


Mchezaji wa Ureno, Renato Sanches ambaye pia ni mchezaji bora wa mchezo huo akijaribu kumtoka mchezaji wa Crotia


Mchezaji wa Croatia PeriÅ¡ić’s ambaye alikuwa kivutio kwa mtindo wa nywele zake. Hata hivyo katika mchezo huo wa leo,licha ya kutegemewa timu yake imeshindwa kufurukuta na kuambulia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Ureno

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here