EPA
Takriban watu 24 sasa wanajulikana kuaga dunia katika mashambulizi mawili tofauti nchini Afghanistan.
14 walikuwa ni maafisa wa ulinzi walio katika mji mkuu Kabul, wakati mshambuliaji wa kujitoa mhanga, alilenga gari la abiria wakati wa masaa yenye shughuli nyingi.
Wizara ya mambo ya ndani inasema kuwa wote wliouawa walikuwa ni raia wa Nepal
Saa chache baadaye, watu 10 waliuawa wakati mkoa ulio kaskazini mwa Badakhshan, wakati bomu lililokuwa limefichwa kwenye pikipiki lilipolipua soko eneo la Kishm.
Taliban na Islamic State wote wanadai kutekeleza mashambulizi ya Kabul.
No comments:
Post a Comment