
Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wametakiwa kutumia sababu kuu zilizosababisha mtikisiko wa umoja wa Ulaya kama changamoto ya kuzidi kuimarisha mashirikiano kati yao ilikujenga jumuiya imara ya Afrika Mashariki itakayokuwa na maslahi mapana ndani ya jumuiya na wananchi kwa ujumla.
Tangu june 24 Uingereza ilipopiga kura ya kujitoa ndani ya jumuiya ya Ulaya, waziri mku wake Davd Cameron naye akijiuzulu, nakuzua mtikisisiko ndani ya jumuiya, wachambuzi wa masuala ya kigeni wanasema viongozi wa Afrika wanaounda jumuiya wanapaswa kuwashirikisha wananchi kila hatua ilikuepuka mgawanyiko.
Wadadi wa biashara za kimataifa wanasema huenda biashara za Afrika zilizokuwa zikifanyika ndani ya umoja wa Ulaya kupitia mgongo wa Uingereza zikadhoofika, huku wakibashiri kuwa huenda Uingereza ikajikita katika kuongeza mahusiano yake na nchi za Marekani na Uchina pamoja na nchi za jumuiya ya madola.
Wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika ya Mashariki wametakiwa kutokuwa na haraka katika kufanikisha shirikisho la kisiasa ndani ya jumuiya, na kwamba wanapaswa kutumia mtikisiko wa jumuiya ya Ulaya kama nyenzo kuu ya kuimarisha ushirikiano ulipo ilikunusuru isivunjike kama 1977.

No comments:
Post a Comment