WANANCHI WA KITUNDA WALIA NA TANESCO . - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, June 30, 2016

WANANCHI WA KITUNDA WALIA NA TANESCO .


Mimi ni Mdau mkubwa sana wa Libeneka hili, na leo nimeona nilete kilio chetu kilio chetu dhidi ya Shirika la Tanesco ambapo naamini kuwa, wahusika wake pia ni wawasomaji wazuri wa libeneke lako hili. Sisi ni Wananchi wakazi wa Mwanagati - Kitunda Block 1 jijini Dar es Salaam na maeneo ya jirani tunatoa malalamiko yetu kwa shirika la TANESCO kwa kutukatia umeme kwa siku tatu mfululizo usiku na mchana.

Tunaliomba shirika la TANESCO lisikilize kilio chetu haraka iwezekanavyo,na kuhakikisha tatizo la umeme linatatuliwa kwa wakati ili kutuepusha na adha tunayoipata hivi sasa sisi wakazi wa Mwanagati Block 1-Kitunda.

Mbali na matatizo hayo, Mji huo ambao ni mpya una chanzo chao cha kipekee na kikubwa cha maji kinachotegemea umeme katika uzalishaji wa maji na kutufanya kukosa maji pia kwa siku 3 mfululizo na kufanya maisha yetu yazidi kuwa magumu zaidi.

Juhudi za kuweza kuwapata wahusika toka shirika la Tanesco ili kuelezea tatizo hili zilishindikana mpaka tunapotoa habari hii, hivyo kupitia libeneke lako pendwa, tunaomba wasikie kilio chetu na kuja kututatulia tatizo hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here