
Watu watatu wamefariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana katika matukio matatu tofauti,huku mmoja akinyofolewa sehemu za siri kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina.
Matukio hayo ya kusikitisha ambayo yameacha simanzi kwa wananchi wa Geita yametokea juzi wilayani Geita kwa nyakati tofauti na katika maeneo tofauti..
Wakizungunza na Channel Ten katika mazishi ya Matangane Kadondo 44 aliyeuawa kwa kitu chenye ncha kali kisha kunyofolewa sehemu zake za siri,baadhi ya wananchi wamelaani mauaji hayo ya kinyama.
Kwa upande wake,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa matukio hayo ambapo amesisitiza kwamba uchunguzi unaendelea kubaini waliofanya mauaji hayo.

No comments:
Post a Comment