Chama cha Soka nchini Uingereza (FA) kimemthibitisha meneja wa klabu ya Sunderland, Sam Allardyce kuwa meneja wa timu ya taifa ya Uingereza.
Kocha mpya wa timu ya taifa ya Uingereza, Sam Allardyce
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 61 amesaini mkataba wa awali wa miaka miwili kufuatia makubaliano na klabu ya Sunderland, aliyoiongoza vyema katika Ligi Kuu msimu uliopita.
Aidha kocha huyo amechukua mikoba ya Roy Hodgson aliyekuwa kocha wa timu hiyo ambaye alijiuzulu baada ya Uingereza kutolewa kwenye michuano ya Euro 2016 na timu ya taifa ya Iceland.
Mchezo wake wa kwanza utakuwa dhidi ya Slovakia tarehe 4 Septemba katika michuano ya kufuzu kuwania kombe la dunia 2018.
Allardyce aliifundisha Sunderland kwa miezi 9 na kuhakikisha haikushuka daraja katika msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment