Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akifanya mazungumzo na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young, alipofika ofisini kwake kwa ajili ya kuzungumza mambo yanayohusu mahusiano ya Tanzania na Korea.Kwa muda mrefu Tanzania imekuwa na urafiki na Korea na katika kulidumisha hilo, Balozi wa Korea nchini, Song Geum-young amemtembelea Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla na kuzungumza mambo mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Korea na Tanzania zaidi katika sekta ya afya na jinsi Korea ambavyo imekuwa ikisaidia uboreshwaji wa huduma za kiafya nchini.
Akizungumza kuhusu ugeni huo, Dk. Kigwangalla alisema kuwa balozi Geum-young alitaka kujua kama naibu waziri anafahamu kuhusu ujenzi wa chuo na hospitali ya Mlonganzira ambapo alitaka kufahamu kama serikali itakuwa tayari kutoa watumishi wa afya 900 ambao watahudumia hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young kuhusu uhusiano wa Tanzania na Korea na jinsi ambavyo nchi hiyo imepanga kuendelea kuisaida Tanzania katika kuboresha huduma za kiafya nchini. (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog)
Katika hilo Dk. Kigwangalla alimuhakikishia balozi kuwa serikali ipo tayari kutoa wataalam wa afya ambao watakuwa wakitoa huduma katika hospitali ya Mlonganzira ambayo itakuwa na vifaa vya kisasa kutoka Korea na itakuwa na vitanda 600 ambavyo vitakuwa vinatumiwa na wagonjwa wanaofika kupata huduma.
Jambo lingine ambalo walizungumza ni kuhusu msaada wa magari ya kutolea huduma za kiafya ambayo yanatembea 'mobile clinic' ambayo yatatolewa kwa kanda zote nchini na zaidi katika maeneo ambayo yanaonekana kuwa na ugumu kufikika na kuwa na vituo vya afya vichache.
Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young, wa kwanza kushoto ni Katibu wa Balozi wa Korea, Songwon Shin na wapili kulia ni Katibu wa Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Kulwa.
"Amesema watatuletea convoy zaidi ya sita (kila moja ina magari 10) ambayo yatagawiwa kwa kila kanda nchini, magari haya kila gari linakuwa na mengine 10 ambayo yanakuwa na huduma mbalimbali za kiafya kama chumba cha upasuaji, store ya madawa, maji na mengine ambayo yanahitajika kutoa huduma kwa mgonjwa," alisema Dk. Kigwangalla.
Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young wakipiga picha ya pamoja baada ya kumaliza mazungumzo.
Aidha aliongeza kuwa magari hayo ya kutolea huduma za afya ambayo yanatembea 'mobile clinic' yanataraji kuletwa nchini mwakani mwezi Januari na kwasasa wizara imetakiwa kuandika andiko la mradi ili kuonyesha kuwa imekubali kuingia katika mradi huo ambao kwa kiasi kikubwa utaweza kurahisisha upatikanaji wa huduma za kiafya kwa maeneo ambayo yana vituo vichache vya afya.
Katibu wa Balozi wa Korea, Songwon Shin akibadilishana mawasiliano na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla katikati ni balozi wa Korea nchini, Song Geum-young.
Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young baada ya kumaliza kufanya mazungumzo.
No comments:
Post a Comment