Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini Marekani, Scott Spencer Storch ameungana tena na Dr Dre baada ya kutangaza kuacha kutumia madawa ya kulevya.
Kabla ya kuingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, Storch aliwahi kutengeneza hits za mastaa kibao akiwemo 2Pac, 50 Cent, Beyonce, Lil Wayne, The Game, Dr. Dre na wengine wengi.
Kupitia akaunti yake ya instagram, Storch aliandika, “One of the best days reunited with @drdre . My brother my family and new chapters with more hits to come . #weworking HISTORY ON REPEAT IN A POSITIVE WAY . #Soberlife
Aidha Storch aliwahi kutajwa kama ni mmoja ya watayarishaji wa muziki matajiri duniani akiwa na utajiri wa $70 milioni lakini mpaka sasa anakadiriwa kuwa na utajiri usiozidi dola milioni 3.6.
No comments:
Post a Comment