Jana usiku Ryan Giggs alionekana akifanya kazi yake mpya ya uchambuzi kwa mara ya kwanza kwenye kituo cha Televisheni cha ITV, akiwa pembeni ya Lee Dixon wakati wakichambua mchezo wa robo fainali ya Euro kati ya Ureno na Poland.
Huku England wakiwa wametupwa nje ya michunao hii mapema kabisa, Giggs aliombwa kutoa maoni yake juu ya kocha anayestahili kubeba mikoba ya kuifundisha England iliyoachwa wazi na Roy Hodgson.
Kwa kuzingatia mahusiano ya karibu ya Giggs na baadhi ya wachezaji na viongozi wa England (Rooney, Neville), ilikuwa ni vigumu kumsikia Giggs ambaye mara nyingi amekuwa si muongeaji mkubwa akitoa kauli kama hii.
Giggs amesema kwamba kufanya vibaya kwa England kunatokana na uatamaduni fulani uliojengeka kwenye taifa hilo, huku akilaumu kitendo cha wachezaji kulipwa pesa nyingi wakati bado hawajapata mafanikio yoyote.
Alipoulizwa je, nani anahisi ni chaguo sahihi la kifundisha Englan baada ya Roy Hodgson kubwaga manyanga?, Giggs alimpendekeza Louis van Gaal kupewa jukumu hilo.
Kauli hiyo imegusa hisia za wengi kutokana na ukweli kwamba wakati wa nyakati za mwisho za Van Gaal United, taarifa zilikuwa zikieleza kuwa hakukuwa na mahusiani mazuri kati ya wawili hao. Lakini kitendo cha Giggs kutoa kauli hiyo kina maana ya kwamba bado anaheshima kubwa juu ya kocha huyo mweye asili ya Kidachi.
No comments:
Post a Comment