Wasiwasi umeongezeka baada ya mgombea mtarajiwa wa chama cha Democrat Hillary Clinton kukutana na kwa zaidi ya masaa matatu na wapelelezi wa FBI kuhusu utumiaji wa barua pepe binafsi kwa matumiziya shughuli za serikali alipokuwa waziri wa mambo ya nje katika serikali ya Obama.
Mkutano wa jumamosi katika makao makuu ya FBI ulikuwa wa khiari. Bi Clinton anataka kuondosha masuala yote juu ya suala hilo ambalo linaonekana halitaki kuondoka.
Bi Clinton alisema, kuwa mara nyingi amekuwa akisema, kuwa kama ningeweza kurudi nyuma, basi ningelishughulikia suala la barua pepe kwa njia tofauti. Ninafahamu kuwa watu wana wasiwasi.
Mgombea mwenziwe mtarajiwa kutoka chama cha Republican, Donald Trump, alikwenda kwenye mtandao wa Twitter, na kuandika; ni vigumu kwa FBI kutokumfungulia mashtaka ya uhalifu Hillary Clinton. Kile alichokifanya kilikuwa ni kosa.
Lakini washirika wa Clinton wanalipinga hilo.
Seneta Brown alisema, hakutakuwa na kufunguliwa mashtaka, na hilo linamaanisha amefanya kile ambacho mawaziri wa mambo ya nje wa zamani wamefanya hapo awali kabla yake.
Naye seneta wa zamani mrepublican Rick Santorium alisema kuwakama yeye hakuwa Hillary Clinton, kama angekuwa naibu waziri ambaye amefanya mambo kama hayo, kwanza mtu huyo angefutwa kazi, na wangekuwa wamefunguliwa mashtaka.
Mahojiano ya Bi Clinton na FBI yamekuja baada ya mzozo kuibuka kufwatia mkutano baina ya mumewe , rais wa zamani Bill Clinton na Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali Loretta Lynch, ambaye analibeba jukumu kwa uchunguzi wa serikali juu ya barua pepe za Hillay Clinton.
Bi Lynch alisema, bila shaka mkutano wake na bw Clinton, unaibuwa maswali mengi na wasiwasi. Bila haka sitofanya tena hivyo. Lakini ulikuwa mkutano wa kawaida.
Kuna sheria ambayo haijaandikwa mjini Washington kuwa ni vyema kwa maafisa kuepuka kuonekana na mienendo katika mibaya inayoweza kuwa na ushawishi.
Trump na warepublican wengine wanasema kuwa kukutana huko kunaonyesha kuwa wizara ya sheria ya serikali ya Obama haiwezi kufanya uchunguzi huru kwa mtu ambaye rais amemuunga mkono.
No comments:
Post a Comment