Mgombea urais wa Democratic, Hillary Clinton akiwa na Seneta Tim Kaine katika moja ya mikutano ya kampeni Julai 14, 2016.
Shirikisha
Kaine mwenye umri wa miaka 58 ni mzaliwa wa Minnesotta. Amesomea sheria katika chuo kikuu cha Havard. Kaine ambaye amewahi kushika wadhifa wa meya, gavana na hivi sasa ni seneta wa Virginia, alianza siasa katika ofisi ya baraza la mji huko Richmond, Virginia mwaka 1994.
Baadaye alichaguliwa kuwa meya wa mji, na baadaye kuchaguliwa kama gavana msaidizi katika jimbo la Virginia mwaka 2002 kabla ya kuwa gavana kamili mwaka 2006.
Kaine ni mwanasiasa mkongwe katika chama cha Democratic ambapo yeye mwenyewe anajielezea kuwa “si mtu mwenye hamasa”. Lakini ni mtu mwenye msimamo wa wastani, na inaelezewa ana uwezo wa kuwavutia wapiga kura ambao wamechefuliwa na Donald Trump na wale ambao bado wana wakati mgumu kumkumbatia Clinton moja kwa moja.
Bi Clinton akiongea na kituo cha televisheni cha CBS kuhusu uteuzi wake wa Kaine kama mgombea mwenza amesema, “hajawahi kushindwa uchaguzi. Alikuwa meya wa daraja la dunia, gavana na seneta na ni mmoja wa maseneta wanaoheshimika sana ambao ninawafahamu.”
Mmoja wa wajumbe maalum wa Democratic kutoka jimbo la Ohio, Jocelyn Bucaro na ambaye pia anamuunga mkono Clinton amesema ni uamuzi wa busara sana ni dhahiri ana ujuzi, maarifa, akili na mwenye uwezo wa kufanya hivyo.
Kaine ambaye anazungumza lugha ya kihispiania kwa ufasaha mkubwa alipumzika kwa takriban mwaka mzima kutoendelea na masomo yake huko Havard ili kufanya kazi kwenye misheni ya kanisa Katoliki na pia alikuwa mwalimu huko Honduras.
Kwa mujibu wa wasifu wake, Kaine aliweza kuuona umaskini ulivyo kwa karibu zaidi alipokuwa Amerika ya Kati. Muda ambao aliishi huko umemsaidia kuunga mkono suala la wahamiaji wasio na makaratasi kupewa uraia wa Marekani – msimamo ambao huenda ukawavutia wapiga walatino.
Mkurugenzi mtendaji wa Mi Familia vvta, Ben Monterros amesema Clinton “amemchagua mgombea mwenza ambaye ana rekodi ya kutetea na kupigania masuala ambayo yanawaathiri jamii ya walatino na taifa letu: uhamiaji, huduma za afya, haki za wanawake na mazingira.
Kabla ya kuchaguliwa kuingia katika baraza la senate la marekani mwaka 2012, kaine alikuwa mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya chama cha democratic.
No comments:
Post a Comment