KANISA LA TAG LAKABIDHI PIKIPIKI 400 KWA WAANGALIZI WA MAKANISA . - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, July 23, 2016

KANISA LA TAG LAKABIDHI PIKIPIKI 400 KWA WAANGALIZI WA MAKANISA .

KANISA la Assemblies of God Tanzania (TAG) limewapatia pikipiki 400 waangalizi wa majimbo 33 nchini ya Kanisa hilo,ili kuwawezesha kufanikisha utekelezaji wa malengo makuu kumi ya dira ya maendeleo ya kanisa hilo,ili ifikapo mwaka 2018, utekelezaji wa malengo hayo yote yawe yamekamilika.

Akizungumza kwa niaba ya waangalizi waliopokea usafiri huo wa pikipiki,Mchungaji Kalebi Patrick Maumbuka wa kanisa la TAG, Ikungi Mkoani Singida alisema usafiri huo wa pikipiki utawasaidia sana kutangaza neno la Mungu kwa haraka zaidi, kwani awali walikuwa wakitegemea usafiri wa mabasi ambayo yalichangia kuwakwamisha kufikisha ujumbe wa neno la mungu kwa wakati muafaka.


Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG, Bwana John Mtokambali (wa kwanza kutoka kulia) akimkabidhi mmoja wa waangalizi wa kanisa wa Mkoani Singida pikipiki kwa ajili ya kuwawezesha kutangaza neon la Mungu kwenye maeneo yao.


Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG, Bwana John Mtokambali akihubiri neno la mungu kwa waumini wa kanisa hilo waliohudhuria kwenye hafla za kuwakabidhi vyombo vya usafiri vitakavyowasaidia kuharakisha kulifikisha neno la mungu.


baadhi ya waumini wa kanisa la TAG wakiwa kwenye hafla ya makabaidhiano ya vyombo vya usafiri vya waangalizi wa makanisa nchini,sherehe hiyo ilifanyika mjini Singida.


Jengo la Kanisa la TAG lililopo katika kata ya Mandewa, wilaya ya Singida mjini kulikofanyika hafla ya kuwakabidhi waangalizi wa makanisa vyombo vya usafiri kwa ajili ya kuharakisha usambazaji wa neon la Mungu kwenye maeneo yao.Picha zote na Jumbe Ismailly

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here