KIGOMA: JESHI LA POLISI WAMEKAMATA SILAHA AINA YA MAGAZINE, MAJAMBAZI WAWILI WAFARIKI DUNIA. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, July 23, 2016

KIGOMA: JESHI LA POLISI WAMEKAMATA SILAHA AINA YA MAGAZINE, MAJAMBAZI WAWILI WAFARIKI DUNIA.

MAJAMBAZI wawili ambao hawajajulikana majina yao, wamefariki dunia wakiwa njiani kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu, kutokana na kuvuja damu nyingi katika miili yao, kutokana na majibizano ya kutupiana risasi na Askari Polisi.

Akizungumza naWaandishi wa habari ofisini kwake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma ACP.Obadia Nselu, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema kuwa tukio hilo limetokea Julai 19 mwaka huu katika barabara kuu ya Wilaya ya Buhigwe-Bukuba, katika eneo la msitu wa koli kata ya Buhigwe tarafa ya Manyovu Mkoani Kigoma.

Aidha kamanda Nselu ameongeza kuwa kupitia majibizano ya risasi na Askari Polisi na majambazi hao, walizidiwa nguvu ndipo idadi ya majambazi isiyojulikana walitokomea na kuingia msituni.

Katika tukio hilo Askari Polisi waliwadhibiti majambazi hao wameweza kukamata silaha moja aina ya SMG yenye namba za usajili 13303136 ikiwa na magazini moja na risasi 16.

Katika tukio lingine, kamanda Nselu ameongeza kuwa kupitia operesheni zinazofanywa na kikosi cha usalama barabarani kwa lengo la kupunguza ajali zisababishazo vifo na majeruhi kwa wananchi, kwa mwaka 2015 kuanzia Januari hadi DesembA jumla ya watu 82 Mkoani Kigoma walifariki dunia kutokana na ajali za barabarani huku jumla watu 122 wakijeruhiwa katika ajali hizo.

Ameongeza kuwa kwa kipindi cha mwaka 2016 kuanzia Januari hadi Juni jumla ya watu 44 wamepoteza maisha yao kutokana na ajali za barabarani huku jumla ya watu 53 wakiwjeruhiwa. 


Kaimu kamanda Mkoani Kigoma ACP, Obadia Nselu akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya tukio la vifo vya majambazi na kukamatwa kwa siraha Mkoani Kigoma leo. 


Baadhi ya pikipiki zilizokamatwa katika operation inayoendelea.


Silaha zilizokamatwa mkoani Kigoma hii leo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here