Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mama’ke mzazi, Lucresia Karugila.
Dar es Salaam: Ni laana? Katika hali ya kushangaza, mwigizaji asiyeonekana lokesheni wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameonesha tabia ya chafu mbele ya mama’ke mzazi, Lucresia Karugila baada ya kuporomosha matusi mazito kufuatia kuhojiwa kuhusu habari ya yeye kudaiwa kuhamia kwa mchumba’ke aishiye Kigamboni jijini Dar.
ISHU YENYEWE
Amani lilipenyezewa ubuyu kuwa mrembo huyo ambaye kinywa chake kimeanza kuzoeleka kwa kutoa matusi ya nguoni, amehamia kwa mpenzi wake huyo ambaye ni bosi wa redio moja maarufu Bongo ndipo paparazi wetu alipoanza kwa kumpigia mama Lulu kisha Lulu akadakia na kuanza kuporomosha matusi mazito.
MAMA ALIANZISHA
Mara baada ya kupokea simu na kuulizwa kuhusu Lulu kujiachia mtandaoni na mwanaume huyo kisha kudaiwa kuhamia Kigamboni, bi’mkubwa huyo aling’aka.
Paparazi: Haloo mama Lulu habari?
Mama Lulu: Salama.
Paparazi: Unaongea na mwandishi wa Global?
Mama Lulu: Ndiyo…
Paparazi: Nakuulizaje, naona Lulu anajiachia mtandaoni na (anatajiwa jina) labda utuambie kama mama yake, process za ndoa zimekaribia? Maana inasemekanaa pia…
Mama Lulu: Haloo…halooo…ninasema kwani ndiye Lulu au ni mimi unaongea na mama Lulu au wewe uliwahi kuzaliwa na mama fulani kwamba unaweza kuwa mama? Au mnajifanyisha?
Paparazi: Kwa sababu mama tumesikia amehamia Kigamboni kwa mchumba wake…
Mama Lulu: Aaa! Nikuulize wewe mtoto…kwani mimi habari…kwanza mimi habari ya Lulu kujiachia na huyo (amtaja mchumba wa Lulu), kwanza mimi huyo (amtaja jina mchumba wa Lulu) simfahamu.
Paparazi: Kwa sababu sisi tumesikia ameamua kuishi naye kabisa Kigamboni…
LULU AWEHUKA SASA
(amnyang’anya simu mama yake)
Lulu: Hata kama nimeenda kuishi naye wewe inakuhusu nini? Halafu wewe mbona unanifuatilia sana (tusi), si ulisema unakwenda kunishtaki.
Paparazi: Eeeh.
Lulu: Eee nini?
Paparazi: Halooo…
Lulu: Hujasikia? Haloo ndiyo hunisikii?
Paparazi: Enhe umesema?
Lulu: Nimeongea, hujasikia nikiongea?
Paparazi: Sijasikia umesemaje yaani labda sijaelewa?
Lulu: Hujaelewa, unataka kuelewa nini, kwanza wewe ni nani mpaka nikueleweshe kwa mfano!
Paparazi: Mimi ni mwandishi…
Lulu: Kwa hiyo kama ni mwandishi nikusaidie nini? Nishakwambia usinifuatilie, nimeenda polisi, sijaenda, haikuhusu!
Paparazi: Aaah…naongea na Lulu siyo?
Lulu: Unaongea na Lulu mwenyewe.
Paparazi: Ahaaa…
Lulu: Ahaa nini?
Paparazi: Lakini mbona ni kitu ambacho kipo wazi hata mtandaoni mnajiachia?
Lulu: Sasa kama umeoona unauliza nini? Nenda mtandaoni angalia. Picha si umeona, unataka kitu gani?
Paparazi: Lakini watu wameenda mbali wanahoji kwamba ndiyo umehamia kabisa kwa mzee Kigamboni?
Lulu: Hata kama tukiishi wote we unataka kujua kama nani (tusi) wewe? Wewe (tusi) kwani wewe baba yangu? (tusi), baba yangu? Baba yangu…(tusi)
Paparazi: Wewe ni staa ndiyo maana nakuuliza.
Lulu: Mambo yangu hayakuhusu, (tusi) kila siku unakuja na jambo jipyaa…(tusi) eeee…eee. Usintafute wewe dada (mwandishi)…mbona pale ofisini mna majanga mbona hamuandiki?
Paparazi: Unajua hivi vitu vinakuja ofisini, sasa viongozi wanatutuma ‘tubalansi’ stori…
Lulu: Unatumwa wewe jini? Unatumwa wewe jini? Nishakuona wewe (tusi), nishasema sitaki kuandikwa kwenye magazeti yenu. Waambie hao viongozi wako na hata wangenipigia wao ningewajibu hivihivi. Wao si wamekutuma na mimi nakutuma nenda kawaambie sitaki kuandikwa kwenye magazeti yenu especially mambo ya udaku.
Mimi nakushauri utafute kazi nyingine ya kufanya kazi ya kufuatilia maisha ya watu nayo kazi? Nakushauri utafute kazi nyingine ya kufanya wewe dada (mwandishi) nenda kawafikishie habari.
UJINGA WAPOTEZEWA
Licha ya Lulu kutukana matusi mengi katika mahojiano hayo ambayo kwa busara hayakustahili kuandikwa gazetini, mhariri aliamua kumpotezea mwigizaji huyo kwani si busara kwa mtu mzima kumsikiliza mtu anayeropoka matusi bila ‘breki’.
NENO LA MHARIRI
Lulu bado ni kinda sana kisanaa, kutukana mbele ya mama yake mzazi, kutukana watu wazima waliomzidi umri ni ishara ya kwamba amekosa mafunzo hivyo ni vyema mama yake akajitathimini upya kuhusu mwenendo wa mwanaye na kuamua kubadili mfumo wa maisha yao kwani asiyefunzwa na wazazi, hufunzwa na ulimwengu.
Hata hivyo, sitaki afunzwe na ulimwengu, namshauri abadilike. Ajifunze upya nidhamu, ajue lugha ya kuzungumza na watu waliomzidi umri. Mimi nimempuuzia aliyoyaongea na kumuona bado ni mtoto anayehitaji kuelimishwa zaidi na ipo siku atakua na kuona alichokifanya ni cha kijinga.
No comments:
Post a Comment