Mambo yanaelekea ukingoni huko Ufaransa, michuano ya Kombe la Ulaya (EURO 2016) inaingia katika hatua ya nusu fainali, ambapo kesho jumatano Julai 06, 2016 timu za taifa, ile ya Wales na ya Ureno zitakabiliana katika hatua hiyo, mtanange utakaopigwa ndani ya dimba la Stade des Rumieres, jijini Lyon, na wapenda soka kote duniani wanasema utakuwa ni mpambano wa magwiji wawili wanaokipiga katika klabu bingwa ya Ulaya 'Real Madrid' yaani Gareth Bale wa Wales na Christian Ronaldo wa Ureno.
Wales watawakosa nyota wake wawili mlinzi Ben Davies anayekipiga Tottenham na kiungo Aaron Ramsey anayekipiga Arsenal wanaotumikia kadi mbili za njano na nafasi zao zikichukuliwa na James Collins na Andy King. Kwa upande wa Ureno wao watamkosa William Carvalho.
Je kocha yupi atacheka au kununa baada ya mwamuzi Jonas Eriksson wa Sweden kupuliza kipyenga cha mwisho ni Chris Coleman wa Wales au Fernando Santos wa Ureno.
No comments:
Post a Comment