KOCHA Mkuu wa timu ya Soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa anatarajia kutangaza kikosi kwa ajili ya kambi ya awali ya wiki moja ikiwa ni maandalizi ya kucheza na Nigeria katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Mkwasa amesema Julai 26 atatangaza kikosi hicho kwa ajili ya kuingia kambini ambapo engo la kambi hiyo itakayoanza Agosti mosi, 2016 ni kuwaweka sawa kisaikolojia wachezaji kabla ya kuita kambi nyingine rasmi wiki ya mwisho ya Agosti kujindaa na mchezo dhidi ya Super Eagles ya Nigeria unaotarajiwa kuchezwa Lagos Septemba 2, mwaka huu.
Taifa Stars ilipangwa kundi G kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambazo zitafanyika Gabon, mwaka 2017. Timu nyingine katika kundi hilo ni Nigeria, Chad na Misri ambayo tayari imefuzu baada ya kukusanya pointi 10, Nigeria ina pointi mbili.
Taifa Stars mpaka sasa ina pointi moja wakati Chad ikijiitoa katikati ya mashindano na kukatisha ndoto za Tanzania kucheza fainali hizo.
No comments:
Post a Comment