MWANASHERIA ALIA NA KUNDI LA IS. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, July 4, 2016

MWANASHERIA ALIA NA KUNDI LA IS.


Mwanasiasa mmoja kutoka katika chama tawala nchini Bangladesh ameeleza masikitiko na hisia za aibu baada ya kugundua kuwa mtoto wake wa kiume ni miongoni mwa kundi la wanamgambo wa kundi la kigaidi la Islamic State walioshambulia mgahawa mmoja katika mji mkuu wa nchi hiyo, Dhaka, mwishoni mwa juma lililopita, na kuua watu ishirini na wawili.

Imtiaz Khan ameiambia BBC kwamba mwanawe huyo wa kiume, aitwaye Rohan, aliondoka nyumbani kwake miezi sita iliyopita.Zaidi ya hayo amewapongeza polisi na serikali ya nchi hiyo kwa kuendesha uchunguzi na hatimaye kumtia mkononi kijana huyo, na amesikitika kusikia kwamba mmoja wa askari polisi aliyekuwa katika harakati za kumkamata kijana huyo alijeruhiwa.

Rohan na wenzake ambao wamefariki dunia wanatoka katika familia maarufu nchini humo na wengine wamesomeshwa ughaibuni.

Khan anamuelezea mwanawe kuwa alikuwa ni kiajana mcha Mungu na mwenye kuzingatia imani yake ya dii ya Kiislamu, na awali hakukuwa na dalili yoyote kwamba siku moja Rohan angekuja kukengeuka na kuwa mwenye itikadi kali kiasi cha kujiunga na kundi hilo la kigaidi.

Kundi la Islamic State lilitupia picha ya Rohan kuwa ndiye aliyetekeleza shambulio hilo, wakati walipokuwa wanatoa tamko la kuhusika na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here