RAIS WA URENO AIKARIBISHA TIMU YA TAIFA - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, July 13, 2016

RAIS WA URENO AIKARIBISHA TIMU YA TAIFA


caption Maelfu ya mashabiki wa timu hiyo walikusanyika katika uwanja wa ndege
Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa ameikaribisha nyumbani timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya kushinda michuano ya Euro 2016.

Maelfu ya mashabiki wa timu hiyo walikusanyika katika uwanja wa ndege mbele ya kasri ya Rais,na katika mitaa ya mji mkuu Lisbon kusheherekea ushindi huo wa kwanza kwa nchi hiyo.
Nahodha wa timu hiyo Cristiano Ronaldo alilipeleka kombe hilo kwenye kasri ya Rais kabla ya kuanza kulitembeza katika mitaa ya jiji la Lisbon wakiwa katika gari la wazi.
Wametajwa kama mashujaa wa nchi hiyo.
Mjini Paris Francois Hollande alikutana na timu ya Ufaransa iliyoshika nafasi ya pili kwenye kasri yake ya Elysee.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here