TAMKO LA RC MAKONDA KUHUSU MASHOGA WALIOPO JIJINI DAR ES SALAAM. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, July 2, 2016

TAMKO LA RC MAKONDA KUHUSU MASHOGA WALIOPO JIJINI DAR ES SALAAM.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza vita na makaka poa (mashoga) na madada poa (makahaba) walioko jijini Dar es Salaam kuwa utaendeshwa msako mkali wa kuwaondoa.

Mkuu wa Mkoa huyo aliyasema hayo kufuatia hali ya vitendo hivyo visiyokubalika na jamii kuzidi kushamiri na kuwa kuna hatari kubwa ya watoto wadogo kuiga vitendo hivyo vinavyoleta picha mbaya kwani ni kinyume na maadili ya mtanzania.

Aidha alisema hawezi kuifumbia macho hali hii kwani inamomonyoa maadali ya jamii na kuwa yuko tayari kulivalia njuga suala hili ili kuhakikisha anawamaliza wote mkoani

Sakati hili la ushoga na ukahaba limeibuka siku za hivi karibuni baada ya kituo cha televisheni cha Clouds Tv kumhoji shoga mmoja ambapo jamii ilipinga kitendo hicho na kuona kama walikuwa wakiuhalalisha ushoga na kuaminisha jamii kuwa ni kitu kizuri.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here