Tunapenda kuwashukuru wazazi na wabunge wote ambao waliotusapoti katika kipindi kigumu cha kuondolewa katika masomo yetu.
Vile vile tunapenda kuchukua mda huu kulaani kitendo cha Serikali kutuondoa chuoni kama mbwa kwa kupewa masaa 24 bila nauli au hela ya kula.
Kiukweli tulifanyiwa ukatili wa hali ya juu ambao ulikuwa ni kinyume cha utawala bora na haki za binadamu.
Dada zetu wamejiuza siku hiyo ili wapate chakula wameondoka na magojwa yasiyotibika kwa sababu ya uzalendo wetu wa kuacha kuendelea na kidato cha 5 na 6 ili tulisaidie taifa letu upungufu wa waalimu wa masomo ya sayansi.
Wazazi wetu wabakia mafukala kwa sababue ya kuuza mashamba yao, ng`ombe zao pamoja kuuza vyakula ghalani kwa sababu ya matarajio yao kuwa sisi tuenda kwenye mfumo ya ajira tutawatunza ila sasa wapata tamaa kabisa.
Sisi tumepoteza mda bure sasa hivi tupo tu mtaan hatujui tunaenda wapi tumeitwa ****** lakini sisi sio ****** kabisa hata tukileta vyeti vyetu sisi vipanga kuliko hata ***** ambae tumemuacha Udom anasoma sema tu sisi wazazi wetu ni wanyonge maskini.
23 July na sisi tutakuwa dodoma kuungana na watanzania wote pamoja na wazazi wetu kifanya mambo yafuatayo;
*Moja*kutoa kilio chetu na maumivu yetu kwa Rais wa awamu ya nne na Mwenyekiti wa ccm taifa juu tulivyonyanyasika na kudhalilisha katika zoezi la Operation tumua watoto wa maskini kwa jina lingine tumeitwa ******.
Tunakuja kumuambia umaskini wa wazazi wetu ndio umetufanya tuitwe ****** na kipindi cha kuomba kura rais aliomba kura mpaka kwa ****** hakuomba kwa vipanga tu.
*Pili*Kupeleka kilio chetu kwa mawaziri wa ccm wa awamu ya nne na kuwauliza ni kwa nini hawakumshauri rais kikwete kuachana na programme hii maana jukumu la rais ni kumshauri rais kwa maana hiyo hata rais wa awamu ya sasa nae alishindwa alikuwa waziri wa ujenzi.
*Tatu*kupeleka kilio chetu kwa wabunge wa ccm ambao walikuwa wengi bungeni kuruhusu programu hii ya special diploma kuengelea na sasa kutugeuka na kutuacha tukifukuzwa kama mbwa na kulala stendi mpaka wabunge wa ukawa kuja kututetea na kututafutia sehemu pa kulala na chakula.
Kuomba hela yetu makazi tuliolipia 182500 na hela ya TCU 20000 na 5000 ya serikali ya wanafunzi walioshindwa kututetea tumesikia tu udomasana daruso ya udsm lakini nyinyi mkaa kimya yetu tuwapei walitutetea nyinsa
*Mwisho* kukabidhi kadi zetu za ccm na za ndugu zetu kama vile mama, baba mjomba shangazi kaka dada na nyinyi kwa mwenyekiti mpya atakae chaguliwa ili kuonyesha maumivu yetu na ndugu zetu kwa unyanyasaji huo tuliofanyiwa.
Vile kuiomba serikali kuturudisha udom ili tumalizie masomo yetu ili tusiwe tumepoteza mda bure maana tumefukuzwa sisi ni kwa sababu ya walimu wetu kudai mshahara yao sio kweli sisi tulikuwa ******.
Special diploma wote 7000 tunaomba tukutane dodoma tarehe 22 ili tujue hatma yetu tarehe 23 July Kwenye mkutano mkuu wa ccm asubuhi na mapema.
No comments:
Post a Comment