Jana ziliripotiwa taarifa kupitia BBC kwamba ndege za kivita za Israeli zimetekeleza msururu wa mashambulizi ya asubuhi mapema huko Gaza Likishambulia maeneo manne yanayohusishwa na wapiganaji wa Hamas.
Huenda ni vyema kuutumia wasaa huu kujuzana KWA KINA NA VINA kuhusu hali halisi ya Ukanda huu wa Gaza
Ukanda wa Gaza (Strong City) ni eneo dogo kwenye mwabao wa Mediteranea ya Mashariki lililopo sehemu ya mamlaka ya Palestina. Lina urefu wa kilomita 40 na upana kati ya 6 km na 14 km. Eneo lote halizidi 360 km². Ni kati ya maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu likiwa na wakazi milioni 1.4 na ni moja ya nchi zinazoongoza kwa msongamano duniani (the most crowded on earth)
Kanda hili ni kati ya mabaki ya Palestina ya Kiingereza yasiyotwaliwa na Israel wakati wa vita ya Kiarabu-Kisraeli ya 1948 na kuwa kimbilio kwa wakimbizi wengi Wapalestina waliowahi kukaa katika sehemu zilizokuwa Israel
1. Gaza imezungukwa katika pande zake zote tatu na Israel ambao wameblock pande hizo zote tatu kwa kutumia jeshi lao la anga na jeshi la majini. Upande wa nne ni borderpoint ya Egypt ambapo jeshi la Misri pamoja na majeshi ya Israeli na lile la wasimamizi wa UN na walinda amani wamefunga njia hizo na yeyote haruhusiwi kutoka ama kuingia ndani ya Gaza.
2. Gaza ni kama gereza kubwa sana ambapo huenda hata sisimizi hana ruhusa ya kuweza kutoka ama kuingia humo bila ruhusa ya Israel. Hii ni kwa sababu wanamgambo Wapalestina maarufu kama HAMAS ambao ndio wanaoongoza Serikali ya nchi hiyo, wanaendelea kurusha roketi ndogo kutoka Gaza kwenda Israel.
3. Gaza haina kiwanja cha ndege, bandari wala hata japo kituo cha treni.
4. Wakazi wa Gaza hawawezi kuondoka nchini mwao kwenda mahali popote kwa kuwa hawana passport . Pia kuna vituo vya ukaguzi vya Israeli kila mahali. Pili hakuna mtu yeyote toka nchi yeyote anayeweza kuingia Gaza pasipokuwa na kibali maalumu ama ruhusa toka kwa serikali ya Israel ambayo hata hivyo pia ni ngumu sana kuipata ruhusa hiyo. Hii pia inawahusu wanasiasa nguli duniani kuingia Gaza ni mbinde. Hata David Cameroon aliwahi kuifananisha Gaza na ‘Kambi ya Wafungwa’ (Prison Camp)
5. Gaza ni sehemu ambayo kiujumla imetenganishwa mbali sana na sehemu kubwa ya nchi zingine za dunia hii haya yamefanywa na israel. Kila siku inayopita bidhaa zote zinazotumika kwa mahitaji ya watu wa Gaza ni lazima zipitie katika vituo vya ukaguzi vya Israeli. Hata maziwa,ngano,madawa na bidhaa zote hupitishwa kwanza katika check point za Israel. Israel hutoza kodi kwa bidhaa zote hizi zinazopita katika vituo vyao vya ukaguzi kwenda Gaza
6. Umoja wa Mataifa UN umewasihi mara kadhaa serikali ya Israel kuondoa vizingiti hivyo na mamlaka yake ndani ya Gaza Israel imekuwa kama sikio la kufa haisikii. Zaidi ya maazimio 50 yamepitishwa na UN dhidi ya Israel lakini Israel hawajali wala kusikiliza.
No comments:
Post a Comment