Habari ya mjini! Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe, anadaiwa kunasa ujauzito wa mwandani wake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ hivyo yupo mbioni kutimiza ndoto yake ya kupata mtoto hivi karibuni.
Jacqueline Wolper Massawe
Habari za uhakika kutoka kwa watu wa karibu wa mastaa hao zilidai kwamba, ishu hiyo ni mpango wa wasanii hao kwa kuwa walipanga mwanzoni wakati wa kuanzisha uhusiano wao hivyo kwa tukio hilo kila mmoja ana furaha na wamejipanga kumpokea mgeni wao.
Chanzo hicho kilimwaga ubuyu kwamba, hivi karibuni, Wolper na Harmonize waliingia kwenye mgogoro kidogo lakini lilipoibuka suala la mrembo huyo kunasa ujauzito, ndipo uhai wa penzi lao ukarejea kwa kiwango cha juu.
“Ni kweli hapo nyuma walizinguana lakini baada ya mimba, sasa hivi penzi lao lipo kwenye ubora wake na kila mmoja anafurahia jambo hilo kwa sababu wamejipanga,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Wikienda lilimsaka Wolper ili kuthibitisha madai hayo ambapo alisema kuwa kama tulivyoipata habari hiyo, kama ni kweli hakuna tatizo lolote yeye kupata ujauzito.
“Jamani habari nyingine ni njema sana, kama kuna mtu amewaambia basi siyo mbaya maana nipo huru kuwa mjamzito kwani sijasababisha chochote kibaya kwa mtu,” alisema Wolper huku Harmonize akisisitiza kuwa Wolper ndiye msemaji pekee wa suala hilo.
No comments:
Post a Comment