WACHEZAJI WA KOREA KASKAZINI NA KUSINI WAPIGA PICHA YA PAMOJA OLIMPIKI RIO 2016. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, August 9, 2016

WACHEZAJI WA KOREA KASKAZINI NA KUSINI WAPIGA PICHA YA PAMOJA OLIMPIKI RIO 2016.

Wanamichezo wa mazoezi ya viungo kutoka Korea Kusini na Kaskazini, ambao wanashiriki Michezo ya Olimpiki Rio 2016, wameuonesha ulimwengu ishara ya umoja, kwa kupiga selfie pamoja.


Picha hii imesifiwa kama ishara ya moyo wa michezo ya Olimpiki 
Lee Eun-ju wa Korea Kusini na Hong Un-jong wa Kaskazini walipiga picha wakiwa wametabasamu wakati wa mazoezi kabla ya kuanza kwa michezo hiyo.

Picha za wanawake hao wawili zimesifiwa sana kwa kuashiria moyo wa Olimpiki wa kuwaleta watu pamoja. Korea Kaskazini na Kusini huwa na uhasama mkubwa.

Uhusiano baina ya nchi hizo mbili umedorora zaidi, kutokana na hatua ya karibuni ya Pyongyang kufanyia majaribio makombora.


Wanamichezo hao walikutana wakati wa raundi ya kufuzu kwa mashindano kamili tarehe 7 Agosti 


Wanamichezo wote wawili hawakufanikiwa kufuzu, lakini bila shaka walibeba ‘dhahabu’ ya uanadiplomasia “Hii ndiyo maana huwa twashiriki Olimpiki,” mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Ian Bremmer aliandika kwenye Twitter na kuweka picha hiyo.

Ujumbe wake ulisambazwa zaidi ya mara 18,000. Wengine hata hivyo hawakufurahishwa na hilo. “Anaruhusiwa kufanya urafiki na adui?”, mmoja wa watu mitandaoni waliuliza, na wengine wakaeleza wasiwasi kwamba huenda Hong akaadhibiwa akirejea nyumbani.

Lee, 17, na Hong, 27, wote walishiriki kama wachezaji wa kufuzu wakiwa binafsi. Ilikuwa mara ya kwanza kwa Lee kushiriki michezo ya Olimpiki.


Lee akishiriki kwenye mashindano ya Olimpiki Rio 


Hong akishiriki mashindano ya Rio tarehe 7 Agosti. Alikuwa mwanamichezo wa kwanza wa mazoezi ya viungo kushindia taifa lake nishani, aliposhinda Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2008. 

Wengi walieleza tofauti iliyopo baina ya wanawake hao wawili na timu ya Olimpiki ya Lebanon iliyokataa kuabiri basi moja na wanamichezo wa Israel.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here