Uwanja wa Amaan mjiniUnguja ni wa kihistoria, japo wengi hawafahamu. Ulijengwa kwa msaada wa serikali ya China na ulifuynguliwa mwaka 1970, ukiwa ni mradi mkubwa wa nchi hiyo wa viwanja vya michezo barani Afrika. Michezo na sherehe nyingi hufanyika uwanjani hapo. Sherehe kubwa ya kihistoria ilifanyika February 5, 1977 wakati vyama vya TANU na Afro Shirazi vilipoungana na kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM. Uwanja huo ulifungwa kwa muda na kufanyiwa ukarabati mkubwa kabla ya kufunguliwa tena mwaka 2010. Una uwezo wa kukaa watu 15,000.
Pia ni uwanja wa kwanza kuweza kuchezewa mechi usiku hapa nchini.
No comments:
Post a Comment