Ni Real Madrid kwa mara ya 3 mfululizo - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, May 27, 2018

Ni Real Madrid kwa mara ya 3 mfululizo


Hakika mtoto mdogo halali na pesa, hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya kile kilichowapata Liverpool hii leo. Pamoja na ubora wao wote walikubali kipigo cha mabao 3 kwa 1 kutoka kwa Real Madrid.

Habari kubwa katika mchezo wa leo ilianza dakika ya 26 baada ya Sergio Ramos kumchezea rafu mbaya Mo Salah ambayo ilimfanya kwenda nje dakika 5 baadae, hata hivyo hadi dakika 45 za kwanza zinaisha ilikuwa Real Madrid 0 Liverpool 0.

Dakika ya 51 uzembe wa mlinda lango wa Liverpool Loris Karius ulimfanya Karim Benzema kuwapa Madrid bao la uongozi, bao hilo lilidumu kwa dakika nne tu kwani mnamo dakika ya 55 Sadio Mane raia wa Senegal aliisawazishia Liverpool goli hilo na Matokeo kusomeka 1-1. Goli la Karim Benzema ni la 56 na anakuwa mchezaji wa pili wa Kifaransa kufunga katika fainali ya Champions League baada ya Zinedine Zidane.

Dakika ya 61 Zinedine Zidane alifanya Mabadiliko kwa kumuingiza Gareth Bale aliyekuwa benchi na sub ya Gareth Bale ilibadili kila kitu katika mchezo huo.

Gareth Bale alifunga mabao mawili, na mabao ya Bale yanamfanya kuwa mchezaji wa kwanza kuingia kama sub na kufunga mara mbili na kuufanya mchezo kumalizika kwa Madrid kuibuka kidedea kwa mabao 3-1 huku Zinedine Zidane akiwa kocha wa kwanza kubeba UEFA Champions League mara tatu mfululizo.

Real Madrid wanakuwa timu ya kwanza kubeba kombe la UCL mara 3 mfululizo baada ya Bayern Munich 1974-1976, na timu za Uingereza sasa zinakuwa zimepoteza katika fainali 7 za mwisho za Ulaya dhidi ya timu kutoka Hispania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here