
Beki Kelvin Yondan akiwaongoza wachezaji wenzake wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuingia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mjini Dar es Salaam kwa safari ya Bujumbura nchini Burundi leo asubuhi
Wachezaji wa Timu ya Taifa wameondoka leo asubuhi Septemba 3, 2019 kuelekea nchini Burundi kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar dhidi ya Burundi mchezo wa Kwanza utachezwa Burundi Septemba 4 na marudiano Uwanja wa Taifa Septemba 8, 2019



Taifa Stars inakwenda Bujumbura kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022

Kipa Juma Kaseja akiingia JNIA kwenda Bujumbura kwa ajili ya mchezo ambao utafanyika kesho

Timu hizo zitarudiana Jumapili Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atapangwa katika moja ya makundi 10 kuanza rasmi mbio za Qatar 2022

Kiungo Mohammed Issa 'Banka' akiingia JNIA leo asubuhi tayari kwa safari

Kipa wa Simba SC, Beno Kakolanya akiwaongoza wenzake kuingia JNIA

Hapa ni wakati wakipata mlo wa asubuhi kabla ya safari yao



No comments:
Post a Comment