Gareth Bale ametolea ufafanuzi juu ya kwanini amebadilisha staili yake ya kupiga mipira ya adhabu na kuamua kutafuta namna nyingine ambayo inaanza kutoa matunda hasa katika michuano ya Euro mwaka huu.
Magoli mawili ya faulo aliyofunga dhidi ya Slovakia na England yamemfanya kulingana na Wafaransa Michel Platini na Zinedine Zidane, na Mjerumani Thomas Hassler.
Endapo atafunga tena dhidi ya Russia leo jijini Toulouse, basi atakuwa amevunja na kuweka rekodi mpya ya kufunga free-kick tatu ndani ya michezo mitatu mfululizo na kuivusha Wales hatua ya mtoano kama watafanikiwa kuibuka na ushindi.
Bale amesema anajiangalia yeye na si kuiga upigaji wa nyota mwenzake wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.
“Nafanya sana mazoezi juu ya suala hili,” alisema Bale
“Hata baada ya mazoezi, natunia dakika 10 mpaka 15 za ziada kupiga faulo kama ambavyo nilikuwa nikifanya Tottenham na sasa Real Madrid,”
Alipoulizwa kama anaiga baadhi ya mbinu kutoka kwa Ronaldo, Bale alisema: “Hapana, si kweli. Mimi nafanya kwa staili yangu mwenyewe na napenda hii staili yangu.
“Ndiyo, ni kweli huwa tunafanya mazoezi pamoja lakini kila mtu hufanya kwa kujitegemea.
“Upigaji wangu unategemea upande niliopo uwanjani.
“Napiga kwa namna tofauti kutegemeana na umbali au ukaribu mpira ulipo.
No comments:
Post a Comment