IBRAHIMOVIC AMESTAAFISHWA SOKA KWA KICHAPO - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, June 23, 2016

IBRAHIMOVIC AMESTAAFISHWA SOKA KWA KICHAPO

Sweden
Bao maridadi la Radja Nainggolan limeiondoa Sweden kwenye mashindano ya mataifa ya Ulaya na kushuhudia mwisho wa Zlatan Ibrahimovic wa soka lake la kimataifa huku Belgium ikifanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
Ushindi huo unaifanya Belgium imalize katika nafasi ya pili ya Kundi E na itakutana na Hungary kwenye mchezo wa 16 bora siku ya Jumapili kwenye mji wa Toulouse.
Nainggolan alifumua shuti kali dakika za lala salama akiwa umbali wa mita 25 na shuti lake kwenda moja kwa moja wavuni na kuitupa Sweden nje ya mashindano.
Sweden imeyaaga mashindano ikiwa na pointi moja baada ya mechi tatu ambazo Ibrahimovic hakufanikiwa kufunga goli hata moja.
  • Goli la Radja Nainggolan ni goli lake la tano kwa Ubelgiji na ni la kwanza tangu October 2015.
  • Ubelgiji wameshinda mechi mbili mfululizo kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Ulaya.
  • Sweden wamepoteza mechi sita kati ya michezo yao nane iliyopita kwenye michuano ya Euro (W1 D1). Wamepata clean sheet moja tu kwenye mechi hizo.
  • Sweden walipiga mashuti manne pekee yaliyolenga goli kwenye mashindano ya mwaka huu, mashuti hayo yalipigwa kwenye mechi yao ya tatu.
  • Shuti la Marcus Berg la dakika ya tano ndiyo lilikuwa shuti la kwanza kwa upande wa Sweden kwenye michuano ya Euro 2016.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here